Friday, 25 August 2023

Mkurugenzi Makumbusho ya Mwalimu Nyerere awapa neno wakazi Kanda ya Ziwa

 

Emmanuel Kiondo, Mkurugenzi Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere-Butiama Mkoani Mara akiwa katika studio za Radio Mazingira Fm. Picha na Edward Lucas

Na Edward Lucas

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Butiama Mkoani Mara, Emmanuel Kiondo awaasa wakazi wa mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa kuwa na tabia ya kutembelea vituo vya utalii

Kiondo ametoa kauli hiyo Alhamisi tarehe 24 Agosti 2023 kupitia kipindi cha Meza ya Michezo kinachorushwa na Mazingira Fm wakati alipofika kuhamasisha mbio za Mwl Nyerere Marathon zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu wilaya ya Butiama.

Amesema kwasasa Makumbusho ya Taifa ya Mwl Nyerere-Butiama yameboreshwa na kuwa ya kisasa zaidi hivyo amewaasa wananchi kutembelea makumbusho hayo kwani kuna mambo mengi ya kujifunza kuhusu historia na urithi wa kihistoria ambao Hayati Mwl Nyerere ameuacha

Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Butiama Mkoani Mara, Emmanuel Kiondo

Thursday, 24 August 2023

Diwani Flaviani Chacha akabidhi sare za CCM kwa Mabalozi kata ya Bunda Stoo

This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-113153-411-1024x768.jpg

This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-111130-6-1024x576.jpg
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Ndugu Gasper Charles mkono wa kushoto akiwa na Diwani Flavian Chacha wakati wa zoezi la kukabidhi sare ya CCM kwa mabalozi kata ya Bunda Stoo
This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-104101-222-1024x768.jpg
This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-110822-967-1024x768.jpg
Mabalozi CCM kata ya Bunda Stoo wakiwa katika ukumbi dakika chache kabla ya kukabidhiwa sare ya CCM na Daftari kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.
This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-115715-771-1024x768.jpg
This image has an empty alt attribute; its file name is img-20230824-115731-272-1024x768.jpg
Mabalozi wa CCM kata ya Bunda Stoo wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa sare ya CCM

Na Edward Lucas

Diwani wa kata ya Bunda Stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara, Mhe. Flavian Chacha Nyamigeko atimiza ahadi yake kwa kuwakabidhi sare ya CCM kwa mabalozi kata ya Bunda Stoo.

Katika hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 24 Agosti 2023 saa 4:00 Asubuhi Ukumbi wa Village kata ya Bunda Stoo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama wakiongozwa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Ndugu Gasper Charles ambapo sambamba na sare hiyo ambayo ni shati mabalozi hao walikabidhiwa pia madaftari na kalamu ili kuwawezesha kutunza kumbukumbu mbalimbali.



Zaidi ya aslimia 95 ya pamba imenunuliwa Bunda

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea, Picha na Adelinus Banenwa

Zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu  na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima wilayani Bunda.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya tani elfu 7 za pamba tayari zimenunuliwa katika vituo vya AMCOS wilayani Bundahuku ikitajwa asilimia 95 ya pamaba tayari imeshanunuliwa kutoka kwa wakulima.

Hayo yamebainishwa na mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea wakati akizungumza na Mazingira fm ofisini kwake ambapo amesema zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu  na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima na zoezi linaendelea vizuri.

Ndugu kabea ameongeza kuwa jukumu lililopo kwa sasa ni wakulima wa zao la pamba kung’olea maotea na kuyachoma moto kama ambavyo maelekezo ya kilimo cha zao hilo yanaelekeza.

mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea

Katika hatua nyingine kabea ameiambia mazingira fm kuwa tayari maelekezo aliyoyaacha  balozi wa pamba Tanzania mhe Aggrey  Mwanri  ya uanzishwaji wa mashamba darasa yameishaanza kufanyiwa kazi ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda tayari mashamba darasa 385 yameanzishwa huku mashamba darasa 180 kwa halmashauri ya mji wa Bunda.

mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea

Mapya yaibuka kifo cha mtoto aliyekutwa kwenye jengo la shule “wazazi wafunguka”

 

Wakazi wa maeneo ya Manyamanyama mtaa wa Mbugani wakiwa eneo ambalo mwili wa mtoto ulikutwa Picha na Adelinus Banenwa

Mwili wa mtoto aliyekutwa amefariki dunia maeneo ya shule ya sekondary ya Ellys iliyoko mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda umetambuliwa.

Na Adelinus Banenwa

Mussa Iramba mkazi wa Hunyari ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo ameiambia Mazingira fm kuwa ni kweli huyo ni mtoto wake anaitwa Suzana Iramba mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kabarimu na kwa kipindi kirefu alikuwa akiishi na shangazi yake maeneo ya majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda,

Mussa amesema taarifa za kifo cha mtoto huyo amezijua kutoka kwa mama yake ambaye alimpigia simu majira ya saa saba za mchana kisha kwenda polisi kutoa maelezo ambapo aliambiwa kwenda chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.

“nimepigiwa simu na maama yake nikiwa hospitali ya DDH kwa kuwa nina mgonjwa anasubili kufanyiwa upasuaji mama yake na huyu mtoto akaniambia suzana amefariki amekutwa kwenye majengo ya shule ya Elly’s nimeshtuka ndipo nilichukua jukumu la kwenda polisi kutoa maeleza na polisi wakaniambia niende kituo cha afya bunda kuutambua mwiuli kama kweli niwamtoto wangu”

Mussa  ameendelea kuiambia mazingira fm akuwa ”ni kweli nimefika kituo cha afya chumba cha kuhifadhia maiti nikakuta kweli ni mwanangu roho inaniuma sana ukiangalia huku ninamgonjwa alafu napata habari kama hizi za msiba ”

Mussa Iramba baba mzazi wa mtoto

Kwa upande wake Estar Boniphas mama mzazi wa suzana amesema taarifa za mtoto huyo kufikwa na umauti alizipata kupitia kwa jeshi la polisi mapema leo asubuhi ambao walikuwa na taarifa za kupotea kwa mtoto huyo tangu tarehe 7 AUGOST ambapo walimwambia afike kituo cha afya bunda na alipofika alipelekwa mojakwa moja chumba cha kuhifadhia maiti ndipo alipogundua mtoto wake amefariki.

Estar Boniphas mama mzazi wa suzana

Radio Mazingira fm ilimtafuta shangazi wa Suzana ambaye ni Mankuru Mlasi mkazi wa mtaa Majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda ambapo amesema taarifa za kifo cha Suzana alizipata tarehe 23 Aug 2023 majira ya saa saba mchana wakati akijiandaa kwenda kumuona mgonjwa wake hospitali.
Wankuru ameiambia mazingira fm kuwa ni kweli yeye amekaa na mtoto Suzana tangua akiwa anasoma darasa la pili hadi amefika darasa la sita na alimchukua kutoka kwa baba yake huko Hunyari na kuanza kuishi naye.
“Ni kweli mtoto huyu nilimchukua kwa baba yake akiwa darasa la pili na nimekaa naye katika kipindi chote hadi amefika darasa la sita lakini amekuwa na tabia ambazo siyo nzuri wakati akiwa kwangu amewahi kuletwa hapa kwangu mara tatu usiku akiwa ameokotwa mtaani siku nyingine aliletwa na mwenyekiti”
Wankuru ameendelea kuiambia mazingira fm kuwa baada ya kuona tabia ya mtoto imezidi hasa ya kushindwa kusoma kutaka kukaa mtaani na udokozi aliamua kumrudisha kwa baba yake huko hunyari na kusaini kwa mwenyekiti kwamba mtoto huyo hayuko tena mikononi mwake.

Wankuru Mlasi shangazi wa Suzana

Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo kata ya Kabarimu amesema ni kweli mtoto huyo anamfahamu na amewahi kuletwa kwake kama mara tatu akiwa ameokotwa mtaani usiku na alikuwa akimrudisha kwa shangazi yake ila kilichoonekana kwa mtoto huyo ni kukataliwa na kukosa malezi kutoka kwa wazazi na ndugu jambo lililopelekea mtoto huyo kuishia mtaani.

Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo

Ikumbukwe kwamba mwili wa suzana iramba ulipatikana tangu jana majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni kwenye jengo moja la shule ya Ellys ambalo halitumiki ukiwa umetelekezwa.

Akutwa amepoteza maisha kwenye pagale ”wananchi wafunguka”

 

Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani wakiwa eneo la tukio , Picha na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Na Adelinus Banenwa

Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara

Mtoto huyo jinsia ya kike amekutwa jioni ya tarehe 22 Augost 2023 na wasamalia wema waliokuwa wakipita karibu na jengo la shule hiyo ambalo kwa Sasa halitumiki Kisha kuujulisha uongozi wa shule ambao pia ulitoa taarifa kwa viongozi wa serikali.

Akizungumza na redio Mazingira fm Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s amesema amepokea taarifa za kuwepo kwa mwili wa mtoto ndani ya Moja ya majengo ya shule ambayo hayatumiki majira ya saa kumi na moja na nusu jioni  na alipofika na kuona uwepo wa mwili huo aliwasiliana na mmiliki wa shule pamoja na viongozi kwa hatua zaidi.

Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s

Naye diwani wa kata ya manyamanyama Mhe Mathayo Machilu ameiambia Mazingira fm kuwa tukio Hilo nilakusikitisha na eneo Hilo la Elly’s limeonekana kuwa hatari kutokana na kuwepo kwa majengo mengi ambayo hayatumiki hivyo yapo kama magofu jambo linaloweza kupelekea uharifu kutendeka.

Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu

Kupitia mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti amewataka wananchi wawe makini na eneo hilo kutokana na muonekano wake pia amewaasa wazazi kuzingatia malezi kwa watoto wao na kufuatilia Kila wanapokwenda ili kuongeza usalama.

Mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti

Wakazi wa mitaa ya nyasura C na Manyamanyama Mbugani wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na hasa maeneo tukio hilo lilipotokea wakidai usalama wake ni mdogo.

Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani

Friday, 18 August 2023

Wakazi idara ya maji Bunda stoo walia ukosefu wa maji

 

Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha mwenye tisheti nyeupe katikati akizungumza na wakaazi wa idara ya maji, Picha na Adelinus Banenwa

Suala la maji katika Mtaa wa idara ya maji hasa maeneo ya panda miti imekuwa ni kikwazo ambapo wamesema hulazimika kuamka usiku wa manane ili kwenda kufata maji.

Na Adelinus Banenwa

Wakazi Mtaa wa idara ya maji kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda wamelalamikia ukosefu wa Maji angali mabomba makubwa ya kusambaza Maji yanapitia katika eneo lao.

Wakizungumza katika kikao kilichohitishwa na Mhe Diwani wa kata hiyo Flavian Chacha wakazi hao wamesema suala la maji katika Mtaa wa idara ya maji hasa maeneo ya panda miti imekuwa ni kikwazo ambapo wamesema hulazimika kuamka usiku wa manane ili kwenda kufata maji.

Aidha wamebainisha kuwa wanalazimika kuchimba mashimo ili kupata maji ambayo kawaidi maji hayo si safi na salama kwa matumizi ya binadamu

Wakazi wa mtaa wa Idara ya Maji wakielezea tatizo la maji
Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha akizungumza na wakazi wa idara ya maji, Picha na Adelinus Banenwa

Akijibu kiro hiyo diwani wa kata hiyo Mhe Flavian amesema serikali kupitia mamlaka ya Maji Bunda inaenda kutekeleza mpango wa kutandaza mabomba ya maji katika maeneo ya Panda miti na maeneo mengine ya kata ya Bunda stoo

Mhe Flavian amesema kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi inasema inakwenda kumtua mama ndoo kichwani hivyo lazima itekelezwe.

Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha

Mbali na suala la maji pia diwani huyo alielezea mipango mingine ya serikali katika kata hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara, shule mpya ya msingi inayogharimu shilingi mil 540, ujenzi hospitali mpya ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa shilingi bil 1.5 miongoni mwa miradi mingine.

Aidha Mhe Flavian amewataka wananchi kujenga tabia ya kuhudhuria mikutano inayoitishwa na Viongozi ili waweze kupata majibu ya maswali yao badala ya kwenda kuzungumzia mtaani.

Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha

Thursday, 17 August 2023

Wakazi wa Misisi Bunda waiomba serikali isaidie kwa hili

 

Nyumba ikiwa na nyufa inayotajwa kusababishwa na ulipuaji wa miamba kwa ajili ya kutengeneza kokoto za ujenzi wa barabara ya Bulamba Nyamuswa. Picha na Edward Lucas

“Serikali itusaidie kampuni ya ujenzi ya China iturekebishie nyumba zetu zilizoharibika wakati wakilipua miamba kutengenezea barabara ya Nyamuswa” wakazi wa Misisi wilaya ya Bunda

Na Edward Lucas

Wakazi wa mtaa wa Misisi kata ya Sazira Halmashauri ya Mji wa Bunda mkoani Mara wameiomba serikali ielekeze na kuisimamia kampuni ya ujenzi ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC), iliyokuwa inajenga barabara ya kipande cha Bulamba Nyamuswa iwafanyie maboresho ya nyumba zao zilizoharibika kutoka na shughuli ya ulipuaji wa miamba ili kupata kokoto za ujenzi wa barabara kutoka katika eneo hilo.

wakazi hao ambao wanaishi karibu na ziliposimikwa mashine za kuchakata kokoto (karasha)wamesema wamejikuta katika mazingira magumu baada ya nyumba zao kubaki na nyufa, mabati kuharibika pamoja na adha zingine jambo linalowasababishia hofu kubwa ya kuendelea kuishi kwenye nyumba hizo

Pius Maiga Ching’oro, Mkazi wa Mtaa wa Misisi akizungumza na Radio Mazingira kuhusu uharibifu wa nyumba zao. Picha na Edward Lucas
Nyakutala Yunza Malembo, mkazi wa Misisi Bunda akielezea changamoto inayowakumba

Mwenyekiti wa mtaa wa Misisi, Amos Mashamba Mgongo amekiri kuwepo kwa malalamiko hayo kutoka katika kaya zipatazo 20 na kueleza kuwa baadhi ya wananchi katika kaya zipatazo 4 walilipwa fidia ili kupisha kwa muda huku wengine wakiahidiwa kufanyiwa marekebisho kutokana na uharibifu utakaokuwa umejitokeza baada ya kumaliza shughuli za ujenzi lakini mpaka sasa hakuna dalili ya kufanyika marekebisho hayo.

Mwenyekiti wa mtaa wa Misisi, Amos Mashamba Mgongo

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mhe. Michael Kweka amesema ni kweli kulikuwepo na malalamiko ya wananchi kupata adha ya vumbi, nyumba kuharibika na changamoto zingine za kiafya ambapo baada ya tathmini baadhi walilipwa ili kupisha kwa muda katika eneo hilo huku akiahidi kufuatilia malalamiko ya wananchi na kuyawasilisha katika mamlaka husika.

Mhe. Michael Kweka, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda ambaye pia ni Diwani wa kata ya Sazira akizungumza na Radio Mazingira Fm kuhusu kilio cha wananchi wa Misisi nyumba kuharibika. Picha na Edward Lucas
Diwani wa kata hiyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda, Mhe. Michael Kweka

Sunday, 13 August 2023

DAS Bunda awa mbogo: aelekeza kuchukuliwa hatua za kinidhamu watumishi wasiyozingatia maelekezo

 

Balozi wa Pamba nchini Aggrey Mwanri mwenye tisheti akiwa na katibu tawala wa Bunda Mhe Salumu Mtelela mwenye shati nyeupe pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya Bunda Picha na Adelinus Banenwa

katibu tawala ameonesha kukerwa na kutoridhika na mahudhurio ya wajumbe katika kikao hicho ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakurugenzi iliwataka watendaji wote kutoka kata na  33 na mitaa na vijiji pamoja na  maafisa ugani kuwepo katika kikao hicho lakini wengi wao hawakufika.

Na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri za mji na wilaya ya Bunda kuwachukulia hatua za kinidhamu watendaji wa kata, mitaa na vijiji ambao balozia wa Pamba alifika katika maeneo yao kutoa elimu lakini wao hawakufika katika kikao cha tathmini.

Balozi wa Pamba nchini Agrei Mwanri mwenye tisheti akiwa na katibu tawala wa Bunda Mhe Salumu Mtelela mwenye shati nyeupe pamoja na baadhi ya wajumbe wa kamati ya usalama ya wilaya ya Bunda Picha na Adelinus Banenwa

Mhe  Mtelela ametoa maagizo hayo leo 12 augost 2023 katika kikao cha tathmini ya ziara ya balozi wa pamba nchini Aggrey Mwanri iliyoanza tangu tarehe 9 mwezi huu na kutamatika kwa kikao hicho cha tathmini

Katika ujumbe wake katibu tawala ameonesha kukerwa na kutoridhika na mahudhurio ya wajumbe katika kikao hicho ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa wakurugenzi iliwataka watendaji wote kutoka kata na  33 na mitaa na vijiji pamoja na  maafisa ugani kuwepo katika kikao hicho lakini wengi wao hawakufika.

Mbali na kuagiza kuchukuliwa kwa hatua za kinidhamu kwa watumishi hao katibu tawala pia amewaagiza watendaji wote wa kata kutoka kata zote 33 za wilaya ya Bunda  kufika ofisini kwake siku ya jumatatu saa tatu asubuhi ili kuweza kuzungumza namna ya kusimamaia itifaki za viongozi pindi maelekezo yanapotolewa.

Katibu tawala wa Bunda Mhe Salumu Mtelela

Kikao cha tathmini ya ziara ya Mhe balozi wa pamba Tanzania Aggrey Mwanri kilitanguliwa na taarifa za wakurugenzi kutoka halmashauri zote mbili za wilaya ya Bunda na taarifa kutoka kwa bodi ya pamaba kupitia kwa mkaguzi wa zao la pamba wilayani Bunda Hemed Kabea

Thursday, 10 August 2023

Salama waibuka mshindi wa tatu Kombe la Samia Jimbo la Bunda

 

Kaptaini wa timu ya Salama akipokea zawadi ya mshindi wa tatu kutoka kwa Mhe. Getere

Timu ya Salama wameibuka mshindi wa tatu katika Kombe la Samia 2023 Jimbo la Bunda kwa kuiburuza timu ya Hunyari goli 3-0 katika viwanja vya shule ya msingi Sarawe.


Magoli ya Salama yamefungwa na John Heziron dakika ya 44' kipindi cha kwanza yakifuatiwa na magoli ya Hemedi Charles na Sanai George dakika ya 60' na 87' kipindi cha pili.


Katika michuano hiyo iliyoratibiwa na Mbunga wa Jimbo la Bunda, Mhe. Boniphace Mwita Getere ilihusisha jumla ya timu 7 kutoka katika Kata zote zinazounda jimbo hilo.


Akitoa zawadi kwa mshindi wa tatu, Mhe. Getere amewaasa vijana kuimarisha urafiki, amani na mshikamano kupitia michezo na kuepuka vitendo vinavyoweza kuleta vurugu na kuwagawa.

Kaptaini wa timu ya Salama akiwa ameshika kiasi cha shilingi 250,000 kama sehemu ya zawadi kwa mshindi wa tatu 

Zawadi kwa mshindi wa tatu ni Jezi, mpira wa miguu na fedha shilingi 250,000.


Fainali itakuwa leo tarehe 10 Agosti 2023 majira ya 10:00 jioni katika viwanja vya Mugeta kati ya Timu ya Mugeta na Ketare



Chama cha wafugaji chatoa msimamo wake uwekezaji bandari

 

Mrida Mshota mwenyekiti wa wafugaji Tanzania, Picha na Adelinus Banenwa

Wafugaji wanaona yapo manufaa makubwa kwenye uwekezaji wa bandari hivyo wanaunga mkono jitihada zote za serikali katika uwekezaji huo.

Na Adelinus Banenwa

Chama cha wafugaji Tanzania kupitia kwa mwenyekiti wake kimesema kinaunga mkono mkataba wa mashirikiano ya serikali na kampuni ya DP World ya Dubai unaohusu uwekezaji katika bandari

Akizungumza msimamo huo wa chama cha wafugaji Tanzania mwenyekiti Mrida Mshota amesema wao kama wafugaji wanaona yapo manufaa makubwa kwenye uwekezaji wa bandari hivyo wanaunga mkono jitihada zote za serikali katika uwekezaji huo.

Sauti Mrida Mshota mwenyekiti wa wafugaji Tanzania

Wakati mwenyekiti wa wafugaji taifa akitoa msimamo huo mahakama kuu kanda ya mbeya leo augost 10  imetupilia mbali shauri la kesi ya kupinga uwekezaji wa bandari iliyofunguliwa mahakamani hapo.