Hakuna kuvumiliana penye hakuna>Mkuu wa Mkoa wa Mara - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 16 May 2018

Hakuna kuvumiliana penye hakuna>Mkuu wa Mkoa wa Mara


Hali mbaya ya miundombinu iliyopo katika kituo cha afya cha Natta kilichopo wilayani Serengeti mkoani Mara kimewaingiza matatani baadhi ya viongozi wa Serikali akiwemo mkurugenzi,Diwani,Mwenyekiti wakijiji pamoja na Daktari kwakushindwa kutoa huduma bora za afya kwa wagonjwa wanaofika kituoni hapo.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoawa Mara Adamu Malima wakati wa Ziara yake wilayani Serengeti alipofika kukagua mradi wa ujenzi unaoendelea katika kituo cha afya cha Natta ndipo kulipobainika changamoto mbalimbali zinazokikabili kituo hicho.

Katika hali isiyodhaniwa kituo hicho hakinaumeme katika baadhi ya maeneo ikiwemo wodi la wazazi jambo ambalo limewalazimu wanawake wanaoenda kujifungua kutumia tochi katika huduma zao zamsingi na hata kwa maeneo muhimu kamachooni pia hakuna umeme.

Dina Joseph mkazi wa kijiji cha Natta amemueleza mkuu wa mkoa kwamba kwa sikumbili sasa tangu afike kituoni hapo hakuna umeme wanalazimika kutumia mwanga wa tochi lakini kwa wale ambao hawana tochi wanatembea gizani jambo ambalo nihatarishi kwamaisha yao.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Mara amesikitishwa na kitendo hicho na kuwaagiza viongozi wanaosimamia kuchukua hatua za haraka kutatua matatizo hayo pasipo kujali itikadi za vyama vyao.No comments:

Post a Comment