Serikali nchini Tanzania imeshauriwa kuchukua hatua
za kisheria kwa wafugaji wanaobainika kuingiza mifugo yao katika hifadhi ya wanyama
na mapori ya akiba badala ya kukamata na
kupiga mnada pasipo kufuata utaratibu stahiki.
Ushauri huo umetolewa hii leo na Musa Gedi Musa
Wakili wa kujitegemea ambae pia ni mwalimu kitaaluma,ambapo amedai hakuna
sheria ya nchi inayoruhusu wafugaji kuuziwa
mifugo yao kiholele isipokuwa ni kuchukuliwa hatua kwa kufikishwa mahakamani .
Amesema ni fedheha kuuzwa kwa shilingi elfu sabini
ng’ombe mwenye thamani ya shilingi laki sita.
Akizungumzia changamoto zinazowakabili wafugaji
kanda ya ziwa na hasa mkoani mara mwenyekiti wa chama cha wafugaji kanda ya
ziwa Mrida mshota amesema kuwa wafugaji wamekuwa kama wahalifu .
Akitolea mfano wa athari ambazo wafugaji wamepata na
takwimu mbalimbali za wafugaji
waliokamatiwa mifugo yao na kuuzwa kwa bei ya chini ikiwemo wilayani Serengeti amedai
zaidi ya ng’ombe 200 walikamatwa wilayani Serengeti na kuuzwa kwa bei ya chini
na kuongeza kuwa mfumo mzima wa mnada uligubikwa na rushwa.
No comments:
Post a Comment