RC Kagera atoa tamko hili juu ya vifo vya mfululizo vya madereva bodaboda - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 17 May 2018

RC Kagera atoa tamko hili juu ya vifo vya mfululizo vya madereva bodaboda

Wananchi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameingia katika hali ya sintofahamu baada ya madereva pikipiki maarufu kama bodaboda kuuawa mfululizo na watu wasiojulikana na wanaachiwa kila kitu walichonacho pamoja na pikipiki zao, hali hiyo inatokea majira ya usiku wanapokodiwa kupeleka abiria.

Akiongea na waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja Jeneral Mstaafu Salum Kijuu amesema kuwa taarifa hizo wameshazipokea na inasemekana ndani ya wiki moja wameuawa madereva pikipiki watatu katika maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo.

No comments:

Post a Comment