Wahamiaji
haramu 236 wamekamatwa mkoani Tanga kwa kuingia nchini bila kibali
katika maeneo mbalimbali kwa kipindi cha Januari hadi Mei 16 mwaka huu.
Kaimu
Ofisa Uhamiaji, Mkoa wa Tanga Salum Farahani amesema hayo leo Mei 16,
wakati akizungumza na Mtanzania Digital na kuongeza kuwa wahamiaji hao
wamekuwa wakiingia mkoani hapa kama njia kuelekea nchini Afrika Kusini.
“Wahamiaji
hao walikamatwa kwa kipindi hicho kwa miezi tofauti tofauti ambapo 49
walikamatwa Januari, 77 walikamatwa Februari, 18 walikamatwa Machi, 26
mwezi Aprili huku 66 wakikamatwa kuanzia Mei mwaka huu.
“Idadi
kubwa ya wahamiaji wanatoka nchini Ethiopia na ndiyo kundi kubwa
linaloongoza kwa kukamatwa ambapo kwa kipindi hicho walikamatwa 140,
wakifuatiwa ambapo wamekuwa wakifika nchini kwa kusafirishwa na
Watanzania ambao nao waliokamatwa.
No comments:
Post a Comment