Wachungaji watatu wanusurika kipigo kwa kushindwa kufufua maiti ya siku 7 - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Wednesday 16 May 2018

Wachungaji watatu wanusurika kipigo kwa kushindwa kufufua maiti ya siku 7

WACHUNGAJI watatu wamenusurika kipigo kutoka kwa wananchi, baada ya kushindwa kumfufua marehemu katika Kijiji cha Sitalike Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.

Wachungaji hao walifika kijijini hapo wakidai kuwa wanao uwezo wa kumfufua marehemu mwanakijiji mwenzao aliyefariki dunia hivi karibuni na kuzikwa kwenye makaburi ya Kijiji hicho.

Akisimulia tukio hilo, mwenyekiti wa kijiji hicho, Christopher Angelo, amesema kuwa tukio hilo lililovuta hisia za watu wengi limetokea Mei 7 kijijini hapo.

Amesema kuwa wachungaji hao ambao walikuwa watatu walifika kwenye ofisi ya Kijiji na kujitambulisha kuwa wao ni wachungaji wanatoka katika Kijiji cha Nsimbo na watakuwapo kijijini hapo wakiwa wameitwa na ndugu wa marehemu, Raymond Mirambo aliyefariki dunia siku moja na kuzikwa kijijini hapo.

Mwenyekiti huyo alisema kutokana na kujitambulisha kwa wachungaji hao kwenye ofisi ya kijiji, uongozi wa kijiji uliwaruhusu wachungaji hao kufanya maombi hayo ya kumfufua marehemu huyo.


No comments:

Post a Comment