Zahanati ya kijiji cha kurusanga iliyopo kata ya Salama wilaya ya Bunda Mkoani Mara kimepokea msaada wa Darubini kutoka kwa Diwani wa Kata ya Ketare - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 24 May 2018

Zahanati ya kijiji cha kurusanga iliyopo kata ya Salama wilaya ya Bunda Mkoani Mara kimepokea msaada wa Darubini kutoka kwa Diwani wa Kata ya Ketare


Zahanati  ya  kijiji cha kurusanga  iliyopo kata ya Salama wilaya ya Bunda  Mkoani  Mara  imepokea  msaada  wa Darubini kutoka kwa Diwani wa Kata ya Ketare mh.Mramba  Simba  Nyamkinda  itakayotumika kupima  magonjwa mbalimbali na kuboresha huduma katika  zahanati  hiyo.

Darubini hiyo  yenye thamani ya shiliingi milioni moja inayotumia nishati ya umeme na jua imetolewa  jana jumamosi na mh.Mramba  Simba  Nyamkinda  ambae ni diwani wa kata ya Ketare baada ya kuona ukosefu wa kifaa hicho katika zahanati hiyo. 

Akizungumza  wakati  wa kupokea kifaa hicho Daktari msimamizi wa Zahanati  hiyo  Sajadi Hassani  amemshukuru mheshimiwa Mramba ambapo amesema awali walikuwa wakitoa huduma kwa kukisia ugonjwa  lakini sasa darubini hiyo itawasaidia kubaini magojwa na kutoa huduma kwa uhakika.

Pia Mramba amemtaka daktari wa kituo hicho kutunza vizuri kifaa hicho  ili kiwasaidie  wananchi kupata huduma za vipimo  ambapo amewaomba  wasikipoteze kama walivyo poteza Darubini aliyoitoa hapo awali.

Wakati huo huo mh.Mramba ametoa pawa miksa katika kanisa la EAGT  la kurusanga na kuahidi kutoa mifuko kumi ya sementi ili kuendeleza ujenzi wa kanisa hilo.

No comments:

Post a Comment