Wafanyabiashara katika soko la
manjebe wamewalalamikia wafanyabiashara wenzao wanaopinga agizo la halmashauri ya mji
wa Bunda likiwataka wafanya biashara wa soko la Nyasura kuhamia manjebe
kwa madai kuwa wanakwamisha biashara zao katika soko hilo.
Wakizungumza na mazingira fm kwa
nyakati tofauti wafanyabiashara katika
soko la manjebe wamesema kuwa serikali itilie
mkazo tamko lake ili wafanyabiashara wajue kuwa soko ni moja tu pia
wafanyabiashara hao wametaka hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi ya wale watakao goma kuhamia
manjebe.
Kwa upande wake Geofrey ambae ni mfanyabiashara
wa samaki katika soko la manjebe amesema kuwa ametekeleza agizo la halimashauri
ya mji lakini wale waliokiuka agizo hilo wamekuwa wanasababisha hali ya kibiashara katika soko
la manjebe kuwa mbaya zaidi.
Aidha Geofrey ametoa wito kwa kusema
kuwa endapo wenzao waliopo soko la nyasura wakikataa kuhamia manjebe ameiomba
serikali kuhamisha tena soko la Nyasura pamoja na soko la Manjebe kwenda
ilikokuwa ofisi ya kijiji kutokana na
eneo hilo kuzungukwa na makazi ya watu na kuwa mzunguko mkubwa wa pesa.
No comments:
Post a Comment