mtaalam kutoka shirika la WWF akiwa katika hatua ya kupimaubora wa maji. Picha na Thomas Masalu
Shirika la WWF kwa kushirikiana na bonde la ziwa Victoria wamefanya zoezi la kupima maji ya mto Tigite uliopo Kijiji cha Matongo Kata ya Matongo wilaya ya Tarime ili kubaini afya ya mto huo katika vigezo vya asili na vya kisayansi.
Na Thomas Masalu
Shirika la WWF kwa kushirikiana na bonde la ziwa Victoria wamefanya zoezi la kupima maji ya mto Tigite uliopo Kijiji cha Matongo Kata ya Matongo wilaya ya Tarime ili kubaini afya ya mto huo katika vigezo vya asili na vya kisayansi.
Zoezi hilo limefanyika leo 26 Sept 2023 ambapo limeshirikisha wadau mbalimbali kama vile vikundi vya watumia maji, wapimaji wa afya ya mto ngazi ya jamii, wanafunzi wa shule ya secondary Matongo na baadhi ya walimu wa shule hiyo.
wadau wakiwa katiaka hatua za upimaji wa maji, Picha na Thomas Masalu
Zoezi lilianza kwa wadau kupewa elimu katika kutambua umuhimu wa upimaji wa maji ya mto, afya ya mto na vifaa vinayotumika kupimia maji ya mto.
Pamoja na hayo wadau walionyeshwa hatua ya kwanza ya upimaji hadi hatua ya mwisho ya upimaji hali iliyo onyesha kufurahiwa na wadau kutokana na kupata maarifa mapya katika utuzanji wa vyanzo vya maji.
Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda (wa kwanza kulia) akiwa ametembelea Banda la WWF katika viwanja vya Sokoine Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara
Mamlaka za serikali na wadau wengine wa Mazingira wametakiwa kudhibiti matumizi ya maji yasiyoendelevu na kudhibiti vyanzo vya maji ili kuulinda Mto Mara
Na Edward Lucas
Maadhimisho ya 12 ya siku ya Mto Mara yamezinduliwa rasmi leo katika Viwanja vya Sokoine mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti mkoani Mara huku wananchi wakitakiwa kuendelea kuutunza Mto Mara kwa kizazi endelevu.
Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo, Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi amesema maadhimisho hayo yanafanyika kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Kenya yaliyopitishwa mwaka 2012 ili kuwa na siku maalumu kila mwaka kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi wa nchi zote mbili kuhifadhi Mto Mara.
Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Mara
Katika Maadhimisho haya yenye kauli mbiu isemayo “Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu” yanakuwa ni ya 6 kufanyika upande wa Tanzania kati ya 12 huku eneo la Mugumu yakiwa yanafanyika kwa mara ya 3 sasa.
Mtanda amesema pamoja na fursa nyingi zilizopo katika bonde la Mto Mara pia limekuwa likikutana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo ya mto.
Amewataka wananchi kuacha vitendo hivyo vinavyoharibu vyanzo vya maji huku akiziagiza mamlaka za serikali na wadau wengine wa Uhifadhi wa Mazingira kusimamia sheria na taratibu zingine zilizoanzishwa ili kuulinda Mto Mara.
Said Mtanda, Mkuu wa mkoa wa Mara
Kilele Cha Maadhimisho ya 12 kitakuwa ni tarehe 15 Septemba 2023 ambapo wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya wanashiriki kuonesha huduma na bidhaa mbalimbali katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti
Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda akiendesha zoezi la upandaji miti na uwekaji wa bikoni kando ya bonde la Mto Mara
Na Edward Lucas
Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda amelipongeza Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira WWF na wadau wengine katika juhudi wanazozifanya katika kuulinda Mto Mara
Mtanda ametoa kauli hiyo leo wakati wa zoezi la upandaji wa miti na uwekaji wa bikoni au vigingi kandokando ya mto Mara katika kijiji cha Borenga Wilaya ya Serengeti katika kuadhimisha siku ya Mto Mara.
Sauti ya Mhe. Mtanda akiwapongeza WWF na wadau wengine kwa Uhifadhi wa mto Mara
Katika zoezi hilo linalotekelezwa maeneo mbalimbali kwenye mkondo wa bonde la Mto Mara, WWF kwa ufadhili wa USAID wamekusudia kupanda miche 44,000 na kuweka vigingi 50 ili kuweka alama zitakazosaidia wananchi kutofanya shughuli zao ndani ya mita 60 katika bonde la mto.
Awali akisoma taarifa fupi ya Uhifadhi wa bonde la Mto Mara, Afisa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Helga Enock Nkongoki amesema jumla ya miti 5000 imeshapandwa eneo la la Nyasurura na Marenge huku miche 500 iliyotolewa na WWF ikipandwa leo eneo la Borenga Serengeti.
Helga Enock Nkongoki akisoma risala ya utekelezaji wa zoezi la upandaji wa miti na uwekaji wa bikoniViongozi na wananchi wakishiriki zoezi la upandaji wa miti 500 eneo la cha Borenga Wilaya ya Serengeti
Viongozi kutoka idara na taasisi mbalimbali wakishirikiana na wananchi kupanda miche na kuweka bikoni kando ya bonde la Mto Mara
Na Edward Lucas
Viongozi kutoka WWF kwa kushirikiana na taasisi zingine pamoja wananchi wameshirikiana kwa pamoja kupanda miche kandokando ya bonde la Mto Mara eneo la kijiji cha Borenga Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.
Sehemu ya banda la WWF katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti maadhimisho ya 12 ya Mto Mara
Kupitia Maadhimisho ya 12 ya siku ya Mto Mara, Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira WWF limeeleza mikakati linayoifanya kuulinda Mto Mara.
Na Edward Lucas
Wananchi mkoani Mara wametakiwa kuendelea kutunza rasilimali ya Mto Mara ili kuifanya kuwa endelevu.
Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mradi WWF mkoa wa Mara, Damas Mbaga wakati akizungumza na Radio Mazingira Fm katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti mkoani Mara katika Maadhimisho ya 12 ya Mto Mara ameeleza ni kwa namna gani wanafanya kuulinda Mto Mara.
Mahojiano ya Mazingira Fm na Mratibu wa Mradi WWF katika Maadhimisho ya 12 ya Mto Mara
Emmanuel Kiondo, Mkurugenzi Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere-Butiama Mkoani Mara akiwa katika studio za Radio Mazingira Fm. Picha na Edward Lucas
Na Edward Lucas
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Butiama Mkoani Mara, Emmanuel Kiondo awaasa wakazi wa mkoa wa Mara na Kanda ya Ziwa kuwa na tabia ya kutembelea vituo vya utalii
Kiondo ametoa kauli hiyo Alhamisi tarehe 24 Agosti 2023 kupitia kipindi cha Meza ya Michezo kinachorushwa na Mazingira Fm wakati alipofika kuhamasisha mbio za Mwl Nyerere Marathon zitakazofanyika mwezi Septemba mwaka huu wilaya ya Butiama.
Amesema kwasasa Makumbusho ya Taifa ya Mwl Nyerere-Butiama yameboreshwa na kuwa ya kisasa zaidi hivyo amewaasa wananchi kutembelea makumbusho hayo kwani kuna mambo mengi ya kujifunza kuhusu historia na urithi wa kihistoria ambao Hayati Mwl Nyerere ameuacha
Mkurugenzi wa Makumbusho ya Taifa ya Mwalimu Nyerere Butiama Mkoani Mara, Emmanuel Kiondo
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Ndugu Gasper Charles mkono wa kushoto akiwa na Diwani Flavian Chacha wakati wa zoezi la kukabidhi sare ya CCM kwa mabalozi kata ya Bunda Stoo
Mabalozi CCM kata ya Bunda Stoo wakiwa katika ukumbi dakika chache kabla ya kukabidhiwa sare ya CCM na Daftari kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.
Mabalozi wa CCM kata ya Bunda Stoo wakiwa na viongozi mbalimbali katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa sare ya CCM
Na Edward Lucas
Diwani wa kata ya Bunda Stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara, Mhe. Flavian Chacha Nyamigeko atimiza ahadi yake kwa kuwakabidhi sare ya CCM kwa mabalozi kata ya Bunda Stoo.
Katika hafla hiyo iliyofanyika leo tarehe 24 Agosti 2023 saa 4:00 Asubuhi Ukumbi wa Village kata ya Bunda Stoo ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama wakiongozwa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Bunda, Ndugu Gasper Charles ambapo sambamba na sare hiyo ambayo ni shati mabalozi hao walikabidhiwa pia madaftari na kalamu ili kuwawezesha kutunza kumbukumbu mbalimbali.
Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea, Picha na Adelinus Banenwa
Zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima wilayani Bunda.
Na Adelinus Banenwa
Zaidi ya tani elfu 7 za pamba tayari zimenunuliwa katika vituo vya AMCOS wilayani Bundahuku ikitajwa asilimia 95 ya pamaba tayari imeshanunuliwa kutoka kwa wakulima.
Hayo yamebainishwa na mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea wakati akizungumza na Mazingira fm ofisini kwake ambapo amesema zoezi la ununuzi wa pamba linaelekea ukingoni tayari kilo million saba na laki tatu na elfu hamsini na sita tayari zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima na zoezi linaendelea vizuri.
Ndugu kabea ameongeza kuwa jukumu lililopo kwa sasa ni wakulima wa zao la pamba kung’olea maotea na kuyachoma moto kama ambavyo maelekezo ya kilimo cha zao hilo yanaelekeza.
mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea
Katika hatua nyingine kabea ameiambia mazingira fm kuwa tayari maelekezo aliyoyaacha balozi wa pamba Tanzania mhe Aggrey Mwanri ya uanzishwaji wa mashamba darasa yameishaanza kufanyiwa kazi ambapo kwa halmashauri ya wilaya ya Bunda tayari mashamba darasa 385 yameanzishwa huku mashamba darasa 180 kwa halmashauri ya mji wa Bunda.
mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda ndugu Hemed Kabea
Wakazi wa maeneo ya Manyamanyama mtaa wa Mbugani wakiwa eneo ambalo mwili wa mtoto ulikutwa Picha na Adelinus Banenwa
Mwili wa mtoto aliyekutwa amefariki dunia maeneo ya shule ya sekondary ya Ellys iliyoko mtaa wa Mbugani kata ya Manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda umetambuliwa.
Na Adelinus Banenwa
Mussa Iramba mkazi wa Hunyari ambaye ni baba mzazi wa mtoto huyo ameiambia Mazingira fm kuwa ni kweli huyo ni mtoto wake anaitwa Suzana Iramba mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Kabarimu na kwa kipindi kirefu alikuwa akiishi na shangazi yake maeneo ya majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda,
Mussa amesema taarifa za kifo cha mtoto huyo amezijua kutoka kwa mama yake ambaye alimpigia simu majira ya saa saba za mchana kisha kwenda polisi kutoa maelezo ambapo aliambiwa kwenda chumba cha kuhifadhia maiti ili kuutambua mwili huo.
“nimepigiwa simu na maama yake nikiwa hospitali ya DDH kwa kuwa nina mgonjwa anasubili kufanyiwa upasuaji mama yake na huyu mtoto akaniambia suzana amefariki amekutwa kwenye majengo ya shule ya Elly’s nimeshtuka ndipo nilichukua jukumu la kwenda polisi kutoa maeleza na polisi wakaniambia niende kituo cha afya bunda kuutambua mwiuli kama kweli niwamtoto wangu”
Mussa ameendelea kuiambia mazingira fm akuwa ”ni kweli nimefika kituo cha afya chumba cha kuhifadhia maiti nikakuta kweli ni mwanangu roho inaniuma sana ukiangalia huku ninamgonjwa alafu napata habari kama hizi za msiba ”
Mussa Iramba baba mzazi wa mtoto
Kwa upande wake Estar Boniphas mama mzazi wa suzana amesema taarifa za mtoto huyo kufikwa na umauti alizipata kupitia kwa jeshi la polisi mapema leo asubuhi ambao walikuwa na taarifa za kupotea kwa mtoto huyo tangu tarehe 7 AUGOST ambapo walimwambia afike kituo cha afya bunda na alipofika alipelekwa mojakwa moja chumba cha kuhifadhia maiti ndipo alipogundua mtoto wake amefariki.
Estar Boniphas mama mzazi wa suzana
Radio Mazingira fm ilimtafuta shangazi wa Suzana ambaye ni Mankuru Mlasi mkazi wa mtaa Majengo kata ya Kabarimu halmashauri ya mji wa Bunda ambapo amesema taarifa za kifo cha Suzana alizipata tarehe 23 Aug 2023 majira ya saa saba mchana wakati akijiandaa kwenda kumuona mgonjwa wake hospitali. Wankuru ameiambia mazingira fm kuwa ni kweli yeye amekaa na mtoto Suzana tangua akiwa anasoma darasa la pili hadi amefika darasa la sita na alimchukua kutoka kwa baba yake huko Hunyari na kuanza kuishi naye. “Ni kweli mtoto huyu nilimchukua kwa baba yake akiwa darasa la pili na nimekaa naye katika kipindi chote hadi amefika darasa la sita lakini amekuwa na tabia ambazo siyo nzuri wakati akiwa kwangu amewahi kuletwa hapa kwangu mara tatu usiku akiwa ameokotwa mtaani siku nyingine aliletwa na mwenyekiti” Wankuru ameendelea kuiambia mazingira fm kuwa baada ya kuona tabia ya mtoto imezidi hasa ya kushindwa kusoma kutaka kukaa mtaani na udokozi aliamua kumrudisha kwa baba yake huko hunyari na kusaini kwa mwenyekiti kwamba mtoto huyo hayuko tena mikononi mwake.
Wankuru Mlasi shangazi wa Suzana
Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo kata ya Kabarimu amesema ni kweli mtoto huyo anamfahamu na amewahi kuletwa kwake kama mara tatu akiwa ameokotwa mtaani usiku na alikuwa akimrudisha kwa shangazi yake ila kilichoonekana kwa mtoto huyo ni kukataliwa na kukosa malezi kutoka kwa wazazi na ndugu jambo lililopelekea mtoto huyo kuishia mtaani.
Mawazo Mussa mwenyekiti wa mtaa wa Majengo
Ikumbukwe kwamba mwili wa suzana iramba ulipatikana tangu jana majira ya saa kumi na moja na nusu za jioni kwenye jengo moja la shule ya Ellys ambalo halitumiki ukiwa umetelekezwa.
Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani wakiwa eneo la tukio , Picha na Adelinus Banenwa
Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara
Na Adelinus Banenwa
Mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 10 hadi 12 amekutwa amefariki na mwili wake kutelekezwa katika jengo Moja la shule ya Elly’s iliyopo mtaa wa mbugani kata ya manyamanyama halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara
Mtoto huyo jinsia ya kike amekutwa jioni ya tarehe 22 Augost 2023 na wasamalia wema waliokuwa wakipita karibu na jengo la shule hiyo ambalo kwa Sasa halitumiki Kisha kuujulisha uongozi wa shule ambao pia ulitoa taarifa kwa viongozi wa serikali.
Akizungumza na redio Mazingira fm Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s amesema amepokea taarifa za kuwepo kwa mwili wa mtoto ndani ya Moja ya majengo ya shule ambayo hayatumiki majira ya saa kumi na moja na nusu jioni na alipofika na kuona uwepo wa mwili huo aliwasiliana na mmiliki wa shule pamoja na viongozi kwa hatua zaidi.
Mariam Chamba mkuu wa shule ya sekondari ya Elly’s
Naye diwani wa kata ya manyamanyama Mhe Mathayo Machilu ameiambia Mazingira fm kuwa tukio Hilo nilakusikitisha na eneo Hilo la Elly’s limeonekana kuwa hatari kutokana na kuwepo kwa majengo mengi ambayo hayatumiki hivyo yapo kama magofu jambo linaloweza kupelekea uharifu kutendeka.
Diwani wa kata ya Manyamanyama Mhe Mathayo Machilu
Kupitia mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti amewataka wananchi wawe makini na eneo hilo kutokana na muonekano wake pia amewaasa wazazi kuzingatia malezi kwa watoto wao na kufuatilia Kila wanapokwenda ili kuongeza usalama.
Mkuu wa kituo cha polisi Bunda OCS Magoti
Wakazi wa mitaa ya nyasura C na Manyamanyama Mbugani wameelezea kusikitishwa na tukio hilo na hasa maeneo tukio hilo lilipotokea wakidai usalama wake ni mdogo.
Wakazi wa mitaa ya Nyasura C na Manyamanyama Mbugani
Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha mwenye tisheti nyeupe katikati akizungumza na wakaazi wa idara ya maji, Picha na Adelinus Banenwa
Suala la maji katika Mtaa wa idara ya maji hasa maeneo ya panda miti imekuwa ni kikwazo ambapo wamesema hulazimika kuamka usiku wa manane ili kwenda kufata maji.
Na Adelinus Banenwa
Wakazi Mtaa wa idara ya maji kata ya Bunda stoo Halmashauri ya Mji wa Bunda wamelalamikia ukosefu wa Maji angali mabomba makubwa ya kusambaza Maji yanapitia katika eneo lao.
Wakizungumza katika kikao kilichohitishwa na Mhe Diwani wa kata hiyo Flavian Chacha wakazi hao wamesema suala la maji katika Mtaa wa idara ya maji hasa maeneo ya panda miti imekuwa ni kikwazo ambapo wamesema hulazimika kuamka usiku wa manane ili kwenda kufata maji.
Aidha wamebainisha kuwa wanalazimika kuchimba mashimo ili kupata maji ambayo kawaidi maji hayo si safi na salama kwa matumizi ya binadamu
Wakazi wa mtaa wa Idara ya Maji wakielezea tatizo la majiMhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha akizungumza na wakazi wa idara ya maji, Picha na Adelinus Banenwa
Akijibu kiro hiyo diwani wa kata hiyo Mhe Flavian amesema serikali kupitia mamlaka ya Maji Bunda inaenda kutekeleza mpango wa kutandaza mabomba ya maji katika maeneo ya Panda miti na maeneo mengine ya kata ya Bunda stoo
Mhe Flavian amesema kupitia ilani ya Chama Cha Mapinduzi inasema inakwenda kumtua mama ndoo kichwani hivyo lazima itekelezwe.
Mhe Diwani kata ya Bunda stoo Flavian Chacha
Mbali na suala la maji pia diwani huyo alielezea mipango mingine ya serikali katika kata hiyo ni pamoja na ujenzi wa barabara, shule mpya ya msingi inayogharimu shilingi mil 540, ujenzi hospitali mpya ya Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa shilingi bil 1.5 miongoni mwa miradi mingine.
Aidha Mhe Flavian amewataka wananchi kujenga tabia ya kuhudhuria mikutano inayoitishwa na Viongozi ili waweze kupata majibu ya maswali yao badala ya kwenda kuzungumzia mtaani.