Thursday, 10 August 2023

Zaidi ya kilo milion 6.9 za pamba tayari zimenunuliwa Bunda

Mkaguzi wa zao la pamba wilayani Bunda Ndugu Hemed kabea, Picha na Adelinus Banenwa

Pamoja na idadi hiyo ya tani za pamba ambazo zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima hadi wakati huu kuonekana ni ndogo lakini bado wakulima wanaendelea kuuza pamba yao katika vituo vya AMCOS hivyo  kufanya mwaka huu kupiga hatua kubwa kulinganisha na miaka mingine iliyopita.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya kilo milioni sita na  laki tisa za pamba sawa tani elfu  sita tayari zimenunuliwa Wilayani  Bunda, kati ya tani elfu 20 zilizokuwa kwenye malengo katika msimu wa mwaka 2022 / 2023

Hayo yamesemwa na mkaguzi wa zao la pamba wilayani Bunda Ndugu Hemed kabea wakati akitoa taarifa ya zao la pamba wilayani Bunda katika kikao kilichowakutanisha maafisa kilimo kutoka Halmashauri zote za Wilaya ya Bunda kikimjumuisha Balozi wa Pamba Nchini Mhe Aggrey Mwanri

Hemedi amesema pamoja na idadi hiyo ya tani za pamba ambazo zimeishanunuliwa kutoka kwa wakulima hadi wakati huu kuonekana ni ndogo lakini bado wakulima wanaendelea kuuza pamba yao katika vituo vya AMCOS hivyo  kufanya mwaka huu kupiga hatua kubwa kulinganisha na miaka mingine iliyopita.

Hemedi amesema kuwa katika msimu wa 2020/ 2021 Bunda ilizalisha pamba tani elfu 4.520 mwaka 2021/2022  Bunda ilizalisha tani elfu 4.546.

Balozi wa pamba Nchini Tanzania Agrei Mwanri, Picha na Adelinus Banenwa

Kwa upande wake balozi wa pamba Nchini Tanzania Aggrey Mwanri amesema katika kuhakikisha zao la pamba linaendelea kufanya vizuri amesema bodi ya pamba imekuja na mpango wa uanzishwaji wa mashamba darasa ambayo yatakuwa chachu kwa wakulima ambapo kwa kila kitongoji kitakuwa na shamba darasa moja la mfano.

Katibu tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela Picha na Adelinus Banenwa

Awali akifungua kikao hicho kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Bunda,  katibu tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela amesema serikali wilayani Bunda inaunga mkono jitihada zote zinazofanywa na bodi ya pamba kwa lengo la kuinua sekta ya pamba wilayani Bunda na ameelekeza watendaji wote Wilaya ya Bunda ngazi za vitongoji , vijiji na mitaa kufanyia kazi maelekezo wanayopewa.

Mtelela: wakulima tumieni teknolojia kwenye kilimo

L
Balozi wa Pamba Nchini Tanzania Aggreyi Mwanri mwenye shati nyeupe akiwa na Katibu tawala Wilaya ya Bunda Mhe Salumu Halfani Mtelela, Picha na Adelinus Banenwa

Wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.

Na Adelinus Banenwa

Akifungua kikao kilichowakutanisha wataalam wa halmashauri zote mbili za wilaya ya Bunda katibu tawala wilaya ya Bunda Salumu Mtelela amewataka wakulima kutumia teknolojia ili kukuza kilimo kama vile kujua ukubwa wa mashamba yao.

Mtelela ameyasema hayo katika kikao cha balozi wa pamba nchini Tanzania AggreyMwanri  ambapo amefika Bunda kwa ajili ya kutoa elimu kwa wakulima namna ya kuandaa mashamba darasa.Picha na Adelinus Banenwa

Sauti ya Salumu Mtelela katibu tawala Bunda

Balozi Aggrey Mwanri amewataka wakulima wa zao la Pamba wilayani Bunda kuachana na kipimo Cha sentimeter 90 kwa 40 kwa kuwa vipimo hivyo vimepitwa na wakati.

Balozi Mwanri amesema wakulima hawapati mazao tarajiwa kwa sababu hawafuati utaratibu wa kilimo bora cha zao la pamba.

Washiriki wa kikao cha zao la pamba, Picha na Adelinus Banenwa

Amesema changamoto kubwa ni wakulima kutopanda pamba kwa  mstari kwa kufuata vipimo vya centemeter 60 kwa 30  pili ni kuchanganya zao la Pamba na mazao Mengine na suala maotea.

Akizungumzia kushuka kwa bei ya pamba nchini balozi Mwanri amesema hii imetokana na bei ya soko ya kidunia huku akiwakumbusha wakulima kuwa serikali haipangi bei ya pamba bali inaweka ukomo wa bei ili kumlinda mkulima.

Sauti ya Balozi wa Pamba Tanzania Aggrey Mwanri

Tuesday, 8 August 2023

Mbunge Getere aendelea kukagua shughuli za maendeleo Jimboni

Mbunge wa Bunda Mhe. Boniface Mwita Getere ameendelea na ziara  kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Jimbo hilo. 




Utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji cha Hunyari kata ya Hunyari ambao umetengewa zaidi ya shilingi milioni 800. Umeanza kujengwa mwezi Machi 2023 na unataegemea kukamilika Agosti 2023





Ujenzi wa Vyumba vitano (5) vya madarasa shule ya msingi Hunyari vyenye thamani ya shilingi milioni 100.


Ujenzi wa barabara ya Nyamatutu hadi Manangasi kiwango cha moramu yenye thamani ya shilingi milioni 74


Na Edward Lucas.

Mbunge wa Jimbo la Bunda Mhe. Boniphace Mwita Getere ameendelea na ziara ya kukagua shughuli za miradi ya maendeleo ndani ya jimbo hilo na kufanya mikutano na wananchi kwa kuwakutanisha na mamlaka husika ili kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miaradi na kujibu hoja za wananchi.

Katika ziara alioifanya jana tarehe 7 Agosti 2023 alitembelea na kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa katika kata ya Hunyari ikiwa ni pamoja na mradi wa maji wenye thamani ya shilingi milioni mia nane ishirini (820, 000,000) unaotekelezwa katika kijiji cha Hunyari ambao ulianza mwezi Machi 2023 na unategemea kukamilika mwezi Agost 2023.

Mhe. Getere alitembelea na kukagua ujenzi wa vyumba vitano vya madarasa katika shule ya msingi Hunyari ambao umekamilika kwa gharama ya shilingi milioni mia moja (100, 000, 000) na ujenzi wa barabara ya Nyamatutu hadi Manangasi kwa kiwango cha moramu yenye thamani ya shilingi milioni sabini na nne (74,000,000)

Aidha Mhe. Getere alihitimisha ziara yake kwa kufanya mkutano na wananchi wa Hunyari katika viwanja vya shule ya msingi Hunyari ambapo katika mkutano huo aliambatana na viongozi kutoka idara na taasisi kama TARURA, RUWASA, TANESCO na ELIMU kwa lengo la kujibu hoja za wananchi na kutoa ufafanuzi wa utekelezaji wa miradi katika eneo hilo.








Sunday, 6 August 2023

Watu 1000 hadi 5000 hupoteza maisha ziwa Victoria kwa mwaka

 

Dkt Masinde Bwire mwenye suti na katibu tawala Bunda Salumu Mtelela mwenye shati nyeusi, Picha na Adelinus Banenwa

Taasisis ya bonde la ziwa Victoria inayohudumia nchi zote ndani ya Afrika Mashariki tayari imeandaa mpango wa kusimika mitambo ya mawasiliano ziwani yenye thamani ya shilingi bilioni 60 pesa ya kitanzania itakayosaidia kutoa taarifa kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa watu wanaotumia ziwa hilo kwa shughuri mbalimbali.

Na Adelinus Banenwa

Zaidi ya watu 1000 hadi 5000 hupoteza maisha kwa kuzama ziwa Victoria kutokana na changamoto mbalimbali zikiwemo ukosefu wa vifaa vya uokozi na mawasiliano.

Hayo yamesemwa na Dkt Masinde Bwire kutoka taasisi ya bonde la ziwa Victoria yenye makao yake makuu jijini Kisumu nchini Kenya.

Akizungumza wakati wa kukabidhi rambirambi kutoka kwenye taasisi hiyo kwa familia zilizopoteza wapendwa wao 14 waliozama ziwa Victoria eneo la Mchigondo kata ya Igundu Halmashauri ya Wilaya ya Bunda mkoani Mara Dkt Bwire amesema kama taasisi tayari wameshaandaa mpango makati wa namna ya kupunguza changamoto ya watu kupoteza maisha ndani ya ziwa.

Katibu Tawala wilaya ya Bunda mwenye shati nyeusia akiwa anatoa ufafanuzi kwa viongozi kabla ya kukutana na wananchi wa Bulomba. Picha na Adelinus Banenwa

Akibainisha mikakati hiyo Dkt Bwire amesema kama taasisis ya bonde la ziwa Victoria inayohudumia nchi zote ndani ya Afrika Mashariki tayari imeandaa mpango wa kusimika mitambo ya mawasiliano ziwani yenye thamani ya shilingi bilioni 60 pesa ya kitanzania itakayosaidia kutoa taarifa kwa changamoto yoyote itakayojitokeza kwa watu wanaotumia ziwa hilo kwa shughuri mbalimbali kama uvuvi, usafiri n.k.

Aidha ameongeza kuwa pia taasisis hiyo inakwenda kutekeleza mpango wa ujenzi wa vituo vya uokozia katika maeneo yanayozunguka ziwa Victoria ambapo kituo kikuu cha kikanda kitajengwa mkoani Mwanza pamoja na vituo vingine vidogo vidoga katika maeneo mengine ikiwemo Musoma ikiwa na lengo la kutoa msaada wa haraka pindi janga linapotokea ziwani.

Dkt Masinde Bwire kutoka taasisi ya bonde la ziwa Victoria

Kwa upande wao wakazi wa kitongoji cha Bulomba kata ya Igundu waishukuru serikali na viongozi wilayani Bunda ikiwa ni pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda ambayo ilikuwa pamoja nao tangu tukio la watu kuzama hadi mtu wa mwisho alipopatikana pia wamelishukuru jeshi la zimamoto na uokoaji kwa kujitoa katika kipindi chote cha kuwatafuta ndugu zao waliokuwa wamezama.

Wakazi wa kitongoji cha Bulomba kata ya Igundu

Aidha wakazi hao wamesema mpango wa kuleta mawasiliano imara ziwani na vituo vya uokoaji utasaidia kwa kiwanbgo kikubwa kuondoa vifo vinavyotokana na watu kuzama majini na kukosa msaada.

Wakazi wa kitongoji cha Bulomba kata ya Igundu

Ghala la pamba la 4C lateketea kwa moto Bunda

Katibu tawala wilaya ya Bunda Mhe Salumu Mtelela Mwenye shati nyeusi, Picha na Adelinus Banenwa

Ghala pamba linalomilikiwa na kampuni ya 4c lateketea kwa moto huku likiwa na mzigo wa pamba ndani, hadi sasa haijulikani hasara ni kiasi gani.

Na Adelinus Banenwa

Katibu tawala wilaya ya Bunda Mhe Salumu Mtelela amesema hadi sasa haijulikani ni kiasi gani cha hasara kutokana na kuungua kwa ghala la pamba katika kiwanda cha 4c kilichoko eneo la viliani Bunda mjini.

Akizungumza katika eneo la tukio hilo Mhe Mtelela amesema yeye kama katibu tawala wilaya alipata taarifa kutoka kwa mkuu wa wilaya juu ya tukio la kiwanda cha pamba kuungua hivyo alichukua hatua za kuwasiliana na kikosi cha zimamoto na uokoaji ambao walifika na kuanza kazi ya kuzima moto huo.

Sehemu ya ghala la pamba iliyoungua
Katibu tawala wilaya ya Bunda Mhe Salumu Mtelela

Aidha amevishukuru vyombo vya usalama ikiwemo jeshi la polisi Bunda kwa kufika mapema kwa ajili ya kuweka ulinzi, pia kikosi cha zimamoto kwa kufika haraka kusaidia kutoa msaada wa kuzima moto huo ambao hadi sasa umedhibitiwa kwa kiasi kikubwa.

Kwa upande wake kamanda wa zimamaoto na uokoaji mkoa wa Mara Agostino Magere amesema jeshi hilo limepata taarifa majira ya saa saba mchana na kikosi hicho kilifika mara moja kudhibiti moto huo.

Aidha Magere ameongeza kuwa changamoto ilikuwa ni maji hata hivyo viongozi wa Bunda walishughulikia changamoto hiyo kwa haraka ambapo amesema taarifa kamili itatolewa baada ya zoezi kukamilika.

Kamanda wa zimamaoto na uokoaji mkoa wa Mara Agostino Magere
Gari la zimamoto likiendelea na kazi ya kuzima moto

Naye mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda Ndugu Hemed Kabea ameiambia mazingira Fm kuwa taarifa za kiwanda kuungua amezipata majira ya saa saba mchana lakini hatua mbalimbali zimefanyika kuhakikisha wanawasiliana na mmiliki wa kiwanda hicho ili kuona namna ya Kudhibiti moto huo .

pia ameishukuru ofisi ya mkuu wa wilaya ya Bunda pamoja na kikosi cha zimamoto na uokoaji mkoa wa Mara kwa kuchukua hatua za haraka ili kupunguza madhara zaidi.

Mkaguzi wa pamba wilaya ya Bunda Ndugu Hemed Kabea

Friday, 4 August 2023

Wenye ulemavu na wanahabari wakutanishwa elimu kupinga ukatili Mara

Dismas Ijagara  mkuu wa Division ya maendeleo ya Jamii wilaya ya Butiama, Picha na Adelinus Banenwa

Dismas amewataka watu wenye ulemavu hasa wanawake na wasichana kujiona watu wa kawaida katika Jamii.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa waandishi wa habari kuelimisha Jamii juu ya madhara yatokanayo ya ukatili wa kijinsia katika Jamii hasa kwa kwa wanawake na wasichana wenye ulemavu.

Akizungumza katika ufunguzi wa warsha ya siku moja iliyofanyika Kyabari wilayani Butiama mkoani Mara Mgeni rasmi Dismas Ijagara mkuu wa Division ya maendeleo ya Jamii wilaya ya Butiama amesema serikali inashirikiana vyema na Asasi za kiraia katika kupambana na ukatili wa kijinsia katika Jamii zetu.

Washiriki wa Warsha ya kupinga ukatili wa kijinsia kwa wenye walemavu

Aidha Ndugu Dismas amewataka watu wenye ulemavu hasa wanawake na wasichana kujiona watu wa kawaida katika Jamii.

Mafunzo haya yamewakutanisha vyama vya wenye ulemavu wilayani Butiama na waandishi wa habari chini ya shirika la C.SEMA na UNFPA kwa ufadhili wa Ubalozi wa Finland chini ya mradi wa “Chaguo langu Haki yangu”.


Mkuu wa  miradi  na Mkurugenzi wa huduma simu kwa mtoto kutoka shirika la C.SEMA Michael Marwa,  Picha na Adelinus Banenwa

Mkuu wa  miradi  na Mkurugenzi wa huduma simu kwa mtoto kutoka shirika la C.SEMA Michael Marwa amesema Lengo kuu la kuwakutanisha vyama vya wenye ulemavu na wanahabari ni kutaka kujenga ulelewa wa pamoja na kutoka na mpango mkakati wa nini cha kufanya kila mtu kwa nafasi yake Ili kuondokana na ukatili huu kwa wanawake na wasichana hasa wenye ulemavu.

Namba 116 yamesaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa taarifa za ukatili

Thelma Dhaje, Meneja huduma ya simu kwa mtoto Tanzania bara, Picha na Adelinus Banenwa.

Lengo la mafunzo haya kati ya Vyama vya wenye ulemavu na waandishi wa habari ni kuweka mpango Kazi wa pamoja na kuweka mapendekezo wa njia gani zitumike katika kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Jamii.

Na Adelinus Banenwa

Katika kukabiliana na matukio ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na wasichana hasa wenye ulemavu shirika la C-SEMA kupitia namba 116 ya huduma kwa mtoto imesaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa taarifa za ukatili katika jamii na wanatarajia kutumia namba hiyo kutuma ujumbe mfupi  sms.

Thelma Dhaje Meneja huduma ya simu kwa mtoto Tanzania bara kutoka shirika la C-SEMA amesema kupitia namba hiyo ya 116 kwa siku hupokea simu hadi 1000 za masuala ya ukatili hivyo kama shirika wameona ufanisi upo kupitia namba hiyo.

Mwenyekiti wa chama cha wenye ulemavu wilaya ya Butiama CHIVAWATA ndugu Jeremah Juma Masungu amesema kupitia mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za umma wilayani Butiama zimekuwa mtari wa mbele katika kutetea haki za wenye ulemavu.

Mkuu wa miradi na mkurugenzi wa huduma ya simu kwa mtoto kutoka shirika la C-SEMA Michael Marwa

kwa upande wake mkuu wa miradi na mkurugenzi wa huduma ya simu kwa mtoto kutoka shirika la C-SEMA Michael Marwa amesema lengo la mafunzo haya kati ya Vyama vya wenye ulemavu na waandishi wa habari ni kuweka mpango Kazi wa pamoja na kuweka mapendekezo wa njia gani zitumike katika kutokomeza ukatili wa kijinsia katika Jamii.

Wednesday, 2 August 2023

Bunda: miili yote 13 yapatikana ajali ya mitumbwi miwili Ziwa Victoria

Kandokando ya Ziwa Victoria eneo la Mchigondo wilaya ya Bunda baada ya ajali ya mitumbwi miwili na kusababisha vifa vya watu 14

 28 walipata ajali 30 July 2023, wakanusurika 14 siku ya tukio , mtoto wa mwaka mmoja akapatikana akiwa amefariki na katika zoezi la utafutaji tarehe 1 August 2023 hadi kufikia saa 12:00 jioni wawili walikuwa wamepatikana na kufika asubuhi 2 August 2023 miili 10 ikawa imepatikana na majira ya saa 6:00 mchana mwili wa mwisho ukapatikana idadi imekamilika 28 zoezi limefungwa.

Na Thomas Masalu

Shughuli ya uokozi katika ajali ya mitumbwi miwili iliyozama ndani ya Ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 14 wilayani Bunda imekamilika baada ya miili yote kuopolewa.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara,  Agostino Magere amesema kazi hiyo imekamilika baada ya mwili wa 13 kuopolewa baada ya takriban siku nne za uokozi.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara,  Agostino Magere

Aidha Magere amebainisha changamoto walizokutana nazo katika utekelezaji wa shughuli hiyo ya uokozi.

Naye kwa upande wake mkuu wa Mkoa wa Mara mheshimiwa Said Mtanda amesema kuwa Rais Dkt .Samia Suluhu ametuma salam za pole kwa wananchi wa mkoa wa Mara kufuatia ajali hiyo.

Breaking News: miili 10 mingine yapatikana ajali ya mitumbwi Bunda

Na Adelinus Banenwa

Katika zoezi la utafutaji ya miili ya wanaoohofiwa kufa maji kwa ajali ya mitumbwi, hadi sasa miili 12 tayari imepatikana kati ya watu 13 waliotajwa kuzama katika ajali hiyo

Baada ya miili miwili kupatikana hada jana jioni, kwa taarifa tulizozipokea asubuhi hii miili mingine 10 imepatikana usiku jana na mingine asubuhi hii na kwasasa imesogozwa kandokando ya Ziwa Victoria eneo la Mchigondo kwa ajili ya utambuzi huku zoezi la kutafuta mwili mwingine likiwa linaendelea.

Indelea kuwa nasi…tutakujulisha zaidi kinachoendelea katika eneo la tukio

Tuesday, 1 August 2023

Mwili mwingine wapatikana waliozama ziwa Victori vifo vyafika 3

wakazi wa vijiji ndani ya kata ya Igundu wakisubili kujua hatma ya ndugu zao wanahofiwa kufa maji, Picha na Adelinus Banenwa

Mwili mwingine wa muumini wa kanisa la KTMK umepatikana jioni hii na kufanya jumla ya waliopatikana kufika wawili huku vifo vikifikia vitatu kati ya watu 28 waliokuwa kwenye mitubwi iliyozama.

Na Adelinus Banenwa

Katika zoezi la utafutaji wa miili ya watu wanaohofiwa kufa maji likiendelea mwili wa mtoto mwingine umepatikana majira ya jioni na kufikisha idadi ya waliothibitika kupoteza maisha kufikia watatu 3  

Mwili uliopatikana jioni hii ni wa Rahel Pius (12) mkazi wa Buwela kijiji cha Igundu ambaye ni mwanafunzi wa darasa la 5 shule ya msingi Bulomba ambaye mwili wake umekabidhiwa kwa familia na mazishi yatafanyika kesho kwa mujibu wa taarifa ya familia.

Waliopatikana leo ni Pendo Charles (13) mkazi wa Sunsi mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Bulomba ambaye tayari mwili wake umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi na Rahel Pius (12) mkazi wa Buwela kijiji cha Igundu ambaye ni mwanafunzi wa darasa la 5 shule ya msingi Bulomba ambaye mwili wake umekabidhiwa kwa familia na mazishi yatafanyika kesho kwa mujibu wa taarifa ya familia.

Mwili wa Pendo ulipatikana majira ya saa saba mchana huku Rahel akipatika majira ya saa 11 jioni

Indelea kufuatilia  taarifa zetu kupata …..updates… ya zoezi linavyokwenda ………….

Bunda: mwili mmoja wapatikana kati ya 13 wanaoohofiwa kufa maji Ziwa Victoria

 

Wananchi wakiwa kandokando ya Ziwa Victoria eneo la Mchigondo Bunda wakiendelea kufuatilia zoezi la utafutaji waliozama. Picha na Adelinus Banenwa

Mwili mmoja umepatikana leo majira ya saa saba mchana katika zoezi la kuwatafuta watu 13 waliozama Ziwa Victoria kijiji cha Mchigondo kata ya Igundu Wilaya ya Bunda.


Na Edward Lucas

Mwili mmoja wapatikana kati ya 13 wanaoohofiwa kufa maji ziwa Victoria katika ajali ya mitumbwi kijiji Mchigondo Bunda na kufanya idadi ya waliofariki kufikia watu 2 mpaka sasa huku zoezi la kuwatafuta wengine 12 likiwa linaendelea.

Aliyepatikana leo majira ya saa saba mchana ni Pendo Charles (13) mkazi wa Sunsi mwanafunzi wa darasa la 7 shule ya Msingi Bulomba ambaye tayari mwili wake umekabidhiwa kwa familia kwa ajili ya kuendelea na shughuli za mazishi.

Akizungumzia zoezi hilo, Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere amesema juhudi za kuwatafuta wengine bado zinaendelea licha ya kukutana na changamoto kadhaa katika zoezi hilo.

Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mara, Agostino Magere