Monday, 19 March 2018

Mtoto wa miaka 14 ajisalimisha polisi kukwepa kuolewa na babu wa miaka 75.


MSICHANA mwenye umri wa miaka 14, amejisalimisha mwenyewe katika Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa akipinga uamuzi wa wazazi wake wa kumuozesha kwa nguvu kwa mzee mwenye umri wa miaka 75, Mtokambali Chele, badala yake anataka apelekwe shule aanze kusoma.

Taarifa za uhakika kutoka eneo la tukio, zinaeleza kuwa baba mzazi wa msichana huyo, Matembezi Mugo, inadaiwa awali alimuozesha dada ya msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 kwa Mzee Chele, lakini alifanikiwa kutoroka kwa mumewe huyo baada ya kubaini kuwa kumbe ni mzee sana. 

Aidha, msichana huyo alibaini kuwa mume wake huyo alikuwa na wake wengine wanne waliomzalia watoto ambao idadi yao inakadiriwa kuwa zaidi ya 50.

Akizungumza na gazeti la Habarileo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, George Kyando alithibitisha kutokea kwa mkasa huo, na kufafanua kuwa msichana huyo alijisalimisha kituoni hapo wiki iliyopita akipinga uamuzi wa wazazi wake kumuozesha kwa nguvu kwa mzee huyo ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Swaila wilayani Nkasi.

 Akisimulia alisema mzazi wa kiume wa msichana huyo, mwishoni mwa mwaka jana alimuozesha binti yake mwenye umri wa miaka 16 kwa Mzee Chele ambaye tayari alikuwa na wake wanne na watoto wanaokadiriwa kufikia 50 na idadi isiyojulikana ya wajukuu na vitukuu.

Majirani wa Mugo ambao kwa masharti ya kutoandikwa majina yao gazetini, walilieleza gazeti hili kwa nyakati tofauti kuwa kuwa alimuozesha binti yake huyo mwenye umri wa miaka 16 kwa mahari ya ng’ombe 50. 

Wanadai kuwa mke wa kwanza wa Mzee Chele ana watoto 14, wa pili ana watoto 13, watatu ana watoto 12 na wanne ana watoto 11. 

“Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 ambaye ni dada yake na huyo msichana mwenye umri wa miaka 14 alipofikishwa nyumbani kwa “mumewe” (Chele) alibaini kuwa ni mzee sana isitoshe tayari alikuwa na wake wanne na watoto wengi tu ...akaamua kutoroka na kukimbilia kusikojulikana,” alieleza Kamanda Kyando.

Aliongeza kuwa baada ya msichana huyo kutoroka nyumbani kwa ‘mumewe’ huyo kijijini Swaila, Mzee Chele alimwendea baba mzazi wa msichana huyo na kumtaka amrejeshe mahari yake yote kwa kuwa binti yake ametoroka nyumbani kwake.

 “Ndipo Mzee Mugo alipomtuliza mzee mwenzake Chele kuwa atampatia binti mwingine ambaye ndiyo huyu mwenyewe miaka 14 akazibe pengo la dada yake aliloliacha nyumbani kwa Mzee Chele baada ya kutoroka... hakuwa tayari kurejesha mahari,” alieleza Kamanda Kyando.

 Aliongeza kuwa kwa usalama wa binti huyo aliyejisalimisha katika Kituo cha Polisi ambako sasa anahifadhiwa kwa muda na Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto la Wilaya ya Nkasi, Anna Kisimba nyumbani kwake. Kutokana na mkasa huo, Kamanda Kyando alithibitisha kuwa tayari Mzee Chele ameshakamatwa.

Jiungeni katika vyama vya ushirika>Waziri Tibeza Bunda Mara


Imeelezwa kuwa Serikali imetangaza utaratibu mpya utakaotumiwa na wakulima wa kilimo cha pamba kuuza zao  hilo  ifikapo msimu wa pamba mapema mwezi mei mwaka huu.

Utaratibu huo umetolewa na waziri wa kilimo Dr.charles  Tizeba  alipokuwa kwenye ziara yake wilayani Bunda mkoani Mara ya kuangalia maandalizi ya masoko  katika msimu wa kuuza kahawa  na pamba unaotarajiwa kuanza mapema mwezi mei.

Dr.Charles  amewasisitizia wakulima wa zao hilo kufata  utaratibu huo  wakujiunga katika vyama vya ushirika vilivyopo katika maeneo yao  kwani atakaye kiuka hataweza kuuza pamba yake mahali popote na kuongeza kuwa utaratibu huo utatumika nchi nzima.

Akitangaza  kuanza kwa msimu wa zao la pamba  waziri Tizeba amesema kuwa msimu utafunguliwa rasmi mei mosi ambapo amewambia  wakulima  wasiwe na wasiwasi kuhusu bei ambayo itatangazwa hivi karibuni.

Saturday, 17 March 2018

Pitia ujuwe Kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Township Rollers leo





                 1. Youthe Rostand
                 2. Juma Abdul
                 3. Gadiel Michael
                 4. Vicent Andrew
                 5. Kelvin Yondani
                 6. Said Juma Makapu
                 7. Yusuph Mhilu
                 8. Papy Tshishimbi
                 9. Obrey Chirwa
                10. Pius Buswita
                11. Thaban Kamusoko

Kikosi cha akiba

12. Ramadhani Kabwili
13. Abdalah Shaibu
14. Nadir Haroub
15. Raphael Daudi
17. Geofrey Mwashiuya
18. Ibrahim Ajibu
19. Juma Mahadhi

Wakili wa Abdul Nondo Afunguka Mazito

                    

Kufuatia sakata la Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Abdul Nonda ambae pia kiongozi wa Mtandao wa Wanafunzi Tanzania TSNP la kudaiwa kutekwa, leo Machi 17 Jebra Kambole ambae ni Wakili wa Mwanafunzi huyo amefunguka na kudai kuwa mpasa sasa hajaonana nae ili kujua kinachoendelea juu yake.

Friday, 16 March 2018

'Nabii anaegawa hela Shillah' azungumza Kanisa kufutiwa usajili.

                

Nabii Daniely Shillah anaegawa hela kanisani kwake amezungumzia kuhusu Kanisa lake kufutiwa usajili. 

Hivi karibuni Nabii Shillah alishika kasi kwenye mitandao ya kijamii ikijinadi kuwa yeye kanisa lake halipo kwa maslahi binafsi.