Thursday, 6 February 2025

 

Kamati ya fedha Bunda TC yakagua miradi, yaipa tano Bunda Mjini Sec

6 February 2025, 

Nyumba ya walimu Bunda mjini Sekondari ambayo itagharimu milion 100 hadi kukamilika kwake

Wananchi watakiwa kulinda miradi ili iweze kudumu na kuhudumia kizazi cha sasa na hata kile kijacho

Na Adelinus Banenwa

Kiasi cha shilingi milioni 88 kimeshatumika kati ya shilingi milioni 100 kwenye ujenzi wa Nyumba ya walimu shule ya sekondari Bunda mjini mkoani Mara

Mkuu wa shule ya sekondari ya Bunda mjini amesema nyumba hiyo imejengwa katika mfumo wa Nyumba mbili ndani ya moja ambayo familia mbili za walimu wataishi pindi itakapokamilika.

Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka, Akisaini kitabu cha wageni baada ya ukaguzi

Ufafanuzi huu umetolewa kwa kamati ya fedha ya halmashauri ya mji wa Bunda iliyofika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa nyumba ya mwalimu.

Katika ujumbe wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka mbali na kupongeza mkuu wa shule kwa usimamizi mzuri wa mradi amemtaka kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili nyumba hiyo iweze kutumika.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka

Kwa upande wake mkurugenzi wa mji wa Bunda Juma Haji ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wailinda miundombinu inayoletwa na serikali katika maeneo yao ili iendelee kuhudumia kizazi cha sasa na hata kijacho.

Sauti ya mkurugenzi wa mji wa Bunda Juma Haji

Monday, 3 February 2025

 

Zaidi ya watu 2700 wafikiwa wiki ya sheria Bunda

3 February 2025, 

Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda, katika kilele wiki ya sheria

Wananchi zaidi ya 2700 wamefikiwa wiki ya sheria wilayani Bunda baada ya kufika katika vituo vilivyokuwa vimeainishwa na wadau wa mahakama.

Na Adelinus Banenwa

Wananchi zaidi ya 2700 wamefikiwa wiki ya sheria wilayani Bunda baada ya kufika katika vituo vilivyokuwa vimeainishwa na wadau wa mahakama.

Hayo yamesemwa na Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda katika kilele cha maadhimisho wiki ya sheria ambapo kwa wilaya ya Bunda maadhimisho hayo yakifanyika leo Feb 3, 2025 kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya ya Bunda.

Sauti ya Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda
Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano katika kilele wiki ya sheria

Katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akiwa mgeni wa heshima ameipongeza mahakama wilayani Bunda kwa kufuata sheria katika kutekeleza majikumu yake hali ambayo amedai inapunguza tabia ya mahakama kulalamikiwa katika utendaji wa haki.

Baadhi aya watumishi wa mahakama wilayani Bunda katika kilele wiki ya sheria

Pia amewashukuru wadau wote wa sheria ikiwemo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ofisi ya mawakili chini ya TLS huku akiwanyooshea vidole baadhi ya mawakili wasiyokuwa waaminifu katika utendaji wao wa kazi .

Sauti Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano

Friday, 31 January 2025

 

Mkurugenzi TECTO community aelezea fursa za ajira kupitia utalii kanda ya ziwa

31 January 2025, 

Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias

Kanda ya ziwa inavivutio vingi vya utalii mbavyo ni fursa Katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira nchini”

Na Catherine Msafiri,

Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias ameeleza kuwa Kanda ya ziwa Kuna fursa nyingi zinazowezakupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii ikiwemo pori la akiba kijereshi ,Hifadhi ya Taifa Serengeti na makumbusho ya baba wa Taifa mwitongo Butiama.

Ameeleza hayo alipofanya mahojiano kwenye kipindi Cha uhifadhi na utalii kinacholushwa kupitia radio Mazingira fm ambapo madam iliangazia juu ya kuvifahamu vivutio vya utalii vinavyopatikana akanda ya ziwa.

Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias akiwa ofisin kwake

Bw. Juma amesema kuwa kama watu wakijikita kuwekeza katika sekta ya utalii itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwakua kuna fursa za biashara za kitalii kama uuzaji wa vinyago ,matunda , utengenezaji wa matenti ya kitalii,vilimo vya utalii na utalii wa kiutamaduni

Sauti ya Juma Elias Mkurugenzi wa TECTO community Company akielezea fursa za kitalii

Aidha ameshauri kuwa watu wanapaswa kujitoa kusoma masuala ya utalii na wale waliosomea wajikite katika vivutio vya Kanda ya ziwa kutasaidia kufungua shughuli za Utalii Kwa ukubwa Kanda ya ziwa

Sauti ya Juma Elias Mkurugenzi wa TECTO community Company akitoa ushauri

Friday, 6 October 2023

Mahafali kidato cha 4 Kabasa Sekondari ni Kambarage tena..!!!!


Ni katika Mahafali ya Kidato cha 4 shule ya Sekondari Kabasa, Kambarage Wasira akiwa mgeni rasmi atoa milioni 1 (1,000,000/=Tsh) kukabili sehemu ya changamoto katika shule hiyo.

Wahitimu wa kidato cha 4 Sekondari Kabasa wakifanya yao mbele ya wageni waalikwa.
Shangwe kama lote kwa walimu na wanafunzi Kabasa Sekondari
Miongoni mwa wageni waalikwa ilikuwa ni pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali wilaya ya Bunda
Kambarage Wasira akizungumza katika mahafali ya 17 shule ya Sekondari Kabasa. Picha na Edward Lucas

Na Edward Lucas

Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Kambarage ashiriki mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Kunzugu na kutoa ahadi ya ‘Printa’ yenye thamani ya milioni 1 na laki 2 (1,200,000/=) hii leo ilikuwa ni zama ya Sekondari Kabasa akiwa mgeni rasmi tena.

Katika mahafali hayo, Kambarage Wasira ametoa shilingi milioni 1 ili kusaidia sehemu ya changamoto zinazoikabiri shule hiyo.

Sauti ya Kambarage Wasira
Godfrey Maige Maduhu, Mkuu wa shule ya Sekondari Kabasa. Picha na Edward Lucas

Awali akisoma taarifa ya shule, Mkuu wa shule hiyo, Godfrey Maige Maduhu amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabiri shule hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bwalo, maktaba, upungufu wa walimu na upungufu wa matundu ya choo 24 huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani shule hiyo ina madarasa ya ziada 6

Sauti ya Godfrey Maige Maduhu
Grace Raymond akisoma risala ya wahitimu kidato cha 4 Sekondari Kabasa ikibainisha baadhi ya changamoto walizokumbana nazo
Sauti ya Grace Raymond

Wednesday, 4 October 2023

NMB yatoa msaada wa dawati 100 Nyasura

 

Baadhi ya viongozi wa NMB na serikali wakipeana mikono baada ya kukabidhi Madawati, Picha na Adelinus Banenwa

Katika kuadhimisha wiki ya wateja banke ya NMB tawi la bunda wametoa msaada wa madawati 100 kwa sule ya msingi ya nyasura iliyopo kata ya nyasura halamshauri ya mji wa bunda mkoani mara.

Na Adelinus Banenwa

Katika kuadhimisha wiki ya wateja banke ya NMB tawi la bunda wametoa msaada wa madawati 100 kwa sule ya msingi ya nyasura iliyopo kata ya nyasura halamshauri ya mji wa bunda mkoani mara.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho amesema banki hiyo imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile sekta ya elimu, afya na uelimishaji wa mambo mbalimbali.

 Amesema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja wamewiwa kutoa msaada huo kwa shule ya Nyasura kutokana na mahitaji yake ambapo dawati 100 zilizotolewa zimegharimu shilingi  12 milioni.

Mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho, Picha na Adelinus Banenwa
Sauti ya mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano ameishukuru bank ya NMB kwa kutoa msaada huo huku akibainisha kwa wilaya ya Bunda inaupungufu wa madawati elfu 16  huku halmashauri ya mji wa Bunda ikiwa na upungufu wa madawati elfu 6 .

Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano, Picha na Adelinus Banenwa
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano,

Kwa upande wake mwalimu  mkuu wa shule ya msingi Nyasura mwalimu Benard Ngero Paul  amesema ujio wa madawati hayo kama msaada kutoka NMB  utapunguza changamoto ya uhaba wa madawati japo bado yanaitajika madawati mengi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi walioko shuleni hapo.

Mwalimu Benard amesema shule ya nyasura ina wanafunzi wapatao 1775 ambapo wasichana ni  985  na wavilana ni 790 ambao wanaitaji madawati 591 huku yaliyopo ni 197 huku upungufu ukitajwa ni madawati 394.

Aidha amebainisha changamoto nyingine ni matundu ya vyoo ambapo kwa mahitaji ni matundu 60 ya vyoo ila yaliyopo ni  12 tu.

Mwalimu  mkuu wa shule ya msingi Nyasura mwalimu Benard Ngero Paul

Tuesday, 26 September 2023

WWF yashirikiana na wadau kupima maji mto Tigite- Tarime

 

mtaalam kutoka shirika la WWF akiwa katika hatua ya kupimaubora wa maji. Picha na Thomas Masalu

Shirika la WWF kwa kushirikiana na bonde la ziwa Victoria wamefanya zoezi la kupima maji ya mto Tigite uliopo Kijiji cha Matongo Kata ya Matongo wilaya ya Tarime ili kubaini afya ya mto huo katika vigezo vya asili na vya kisayansi.

Na Thomas Masalu

Shirika la WWF kwa kushirikiana na bonde la ziwa Victoria wamefanya zoezi la kupima maji ya mto Tigite uliopo Kijiji cha Matongo Kata ya Matongo wilaya ya Tarime ili kubaini afya ya mto huo katika vigezo vya asili na vya kisayansi.

Zoezi hilo limefanyika leo 26 Sept 2023 ambapo limeshirikisha wadau mbalimbali kama vile vikundi vya watumia maji, wapimaji wa afya ya mto ngazi ya jamii, wanafunzi wa shule ya secondary Matongo na baadhi ya walimu wa shule hiyo.

wadau wakiwa katiaka hatua za upimaji wa maji, Picha na Thomas Masalu

Zoezi lilianza kwa wadau kupewa elimu katika kutambua umuhimu wa upimaji wa maji ya mto, afya ya mto na vifaa vinayotumika kupimia maji ya mto.

Pamoja na hayo wadau walionyeshwa hatua ya kwanza ya upimaji hadi hatua ya mwisho ya upimaji hali iliyo onyesha kufurahiwa na wadau kutokana na kupata maarifa mapya katika utuzanji wa vyanzo vya maji.

Thursday, 14 September 2023

Maadhimisho ya 12 ya Mto Mara yazinduliwa rasmi leo


Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda (wa kwanza kulia) akiwa ametembelea Banda la WWF katika viwanja vya Sokoine Maadhimisho ya Siku ya Mto Mara

Mamlaka za serikali na wadau wengine wa Mazingira wametakiwa kudhibiti matumizi ya maji yasiyoendelevu na kudhibiti vyanzo vya maji ili kuulinda Mto Mara


Na Edward Lucas

Maadhimisho ya 12 ya siku ya Mto Mara yamezinduliwa rasmi leo katika Viwanja vya Sokoine mjini Mugumu Wilaya ya Serengeti mkoani Mara huku wananchi wakitakiwa kuendelea kuutunza Mto Mara kwa kizazi endelevu.


Akizungumza katika uzinduzi wa maadhimisho hayo, Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda ambaye ndiye aliyekuwa mgeni rasmi amesema maadhimisho hayo yanafanyika kufuatia uamuzi wa Baraza la Mawaziri kutoka Serikali ya Tanzania na Kenya yaliyopitishwa mwaka 2012 ili kuwa na siku maalumu kila mwaka kwa lengo la kuelimisha na kuhamasisha wananchi wa nchi zote mbili kuhifadhi Mto Mara.

Said Mtanda, Mkuu wa Mkoa wa Mara

Katika Maadhimisho haya yenye kauli mbiu isemayo “Hifadhi Mto Mara kwa Ustawi wa Viumbe Hai na Uchumi Endelevu” yanakuwa ni ya 6 kufanyika upande wa Tanzania kati ya 12 huku eneo la Mugumu yakiwa yanafanyika kwa mara ya 3 sasa.


Mtanda amesema pamoja na fursa nyingi zilizopo katika bonde la Mto Mara pia limekuwa likikutana na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na uchafuzi na uharibifu wa vyanzo vya maji kutokana na shughuli za kilimo na ufugaji katika maeneo ya mto.


Amewataka wananchi kuacha vitendo hivyo vinavyoharibu vyanzo vya maji huku akiziagiza mamlaka za serikali na wadau wengine wa Uhifadhi wa Mazingira kusimamia sheria na taratibu zingine zilizoanzishwa ili kuulinda Mto Mara.

Said Mtanda, Mkuu wa mkoa wa Mara

Kilele Cha Maadhimisho ya 12 kitakuwa ni tarehe 15 Septemba 2023 ambapo wadau mbalimbali kutoka Tanzania na Kenya wanashiriki kuonesha huduma na bidhaa mbalimbali katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti 

Wednesday, 13 September 2023

Mtanda awapongeza WWF kwa Uhifadhi wa Mto Mara


Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda akiendesha zoezi la upandaji miti na uwekaji wa bikoni kando ya bonde la Mto Mara

Na Edward Lucas

Mkuu wa mkoa wa Mara, Said Mtanda amelipongeza Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira WWF na wadau wengine katika juhudi wanazozifanya katika kuulinda Mto Mara

Mtanda ametoa kauli hiyo leo wakati wa zoezi la upandaji wa miti na uwekaji wa bikoni au vigingi kandokando ya mto Mara katika kijiji cha Borenga Wilaya ya Serengeti katika kuadhimisha siku ya Mto Mara.

Sauti ya Mhe. Mtanda akiwapongeza WWF na wadau wengine kwa Uhifadhi wa mto Mara

Katika zoezi hilo linalotekelezwa maeneo mbalimbali kwenye mkondo wa bonde la Mto Mara, WWF kwa ufadhili wa USAID wamekusudia kupanda miche 44,000 na kuweka vigingi 50 ili kuweka alama zitakazosaidia wananchi kutofanya shughuli zao ndani ya mita 60 katika bonde la mto.


Awali akisoma taarifa fupi ya Uhifadhi wa bonde la Mto Mara, Afisa Mazingira Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Helga Enock Nkongoki amesema jumla ya miti 5000 imeshapandwa eneo la la Nyasurura na Marenge huku miche 500 iliyotolewa na WWF ikipandwa leo eneo la Borenga Serengeti.

Helga Enock Nkongoki akisoma risala ya utekelezaji wa zoezi la upandaji wa miti na uwekaji wa bikoni
Viongozi na wananchi wakishiriki zoezi la upandaji wa miti 500 eneo la cha Borenga Wilaya ya Serengeti

Zoezi la Upandaji wa Miti katika bonde la Mto Mara linaendelea


Viongozi kutoka idara na taasisi mbalimbali wakishirikiana na wananchi kupanda miche na kuweka bikoni kando ya bonde la Mto Mara

Na Edward Lucas

Viongozi kutoka WWF kwa kushirikiana na taasisi zingine pamoja wananchi wameshirikiana kwa pamoja kupanda miche kandokando ya bonde la Mto Mara eneo la kijiji cha Borenga Wilaya ya Serengeti mkoani Mara.

Tuesday, 12 September 2023

WWF: ‘Mto Mara ulindwe na Utunzwe’


Sehemu ya banda la WWF katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti maadhimisho ya 12 ya Mto Mara

Kupitia Maadhimisho ya 12 ya siku ya Mto Mara, Shirika la Kimataifa la Uhifadhi wa Mazingira WWF limeeleza mikakati linayoifanya kuulinda Mto Mara.

Na Edward Lucas

Wananchi mkoani Mara wametakiwa kuendelea kutunza rasilimali ya Mto Mara ili kuifanya kuwa endelevu.

Wito huo umetolewa na Mratibu wa Mradi WWF mkoa wa Mara, Damas Mbaga wakati akizungumza na Radio Mazingira Fm katika viwanja vya Sokoine Wilaya ya Serengeti mkoani Mara katika Maadhimisho ya 12 ya Mto Mara ameeleza ni kwa namna gani wanafanya kuulinda Mto Mara.

Mahojiano ya Mazingira Fm na Mratibu wa Mradi WWF katika Maadhimisho ya 12 ya Mto Mara