Tuesday, 16 January 2018

Serikali yaahidi kula sahani moja na watumishi wezi Mkoani Mara



WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia hapo hapo.

 Amesema Serikali haikotayari kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe, hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa uadilifu.

 Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na watumishi wa wilaya ya Musoma mkoani Mara akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku sita mkoani hapa.

 Waziri Mkuu amewasisitiza watumishi wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sharia kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia kupunguza kasi ya kuwaletea maendelea Watanzania.

 Amesema lengo ni kuhakikisha adhima ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan wale wa hali ya chini inatimia, hivyo amewaagiza viongozi wa halmashauri wakiwemo Madiwani kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.

 Pia Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa ofisini na dabala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.

 Waziri Mkuu amesema watendaji hao wanatakiwa waachane na tabia ya kuwasubiri wananchi wawapelekee malalamiko yao kwa sababu baadhi yao hawana uwezo wa kufika katika ofisi zao.

Sunday, 14 January 2018

Watu 40 Watiwa Mbaroni kwa Tuhuma za Mauaji ya Watu Wawilii Mkoani Mara



Jeshi la Polisi mkoa wa Mara linawashikilia watu zaidi ya  40, wakazi wa Kijiji cha Mikomariro wilayani Bunda kwa tuhuma za mauaji ya watu wawili sababu ikitajwa kuwa ni mgogoro wa mpaka wa shamba.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jafari Mohamed amethibitisha kukamatwa kwa watu hao huku akiongeza kuwa Jeshi lake bado linawasaka watu wengine waliohusika na tukio la mauaji ya watu wawili wakazi wa Kijiji cha Remng'orori wilayani Serengeti.

Aidha kamanda Jafari amebainisha kuwa waliokamatwa ni wale walioshiriki yowe iliyosababisha mauaji ya watu wawili kwa kuwakata kwa mapanga kwa sababu ya ugomvi wa mipaka ya mashamba.

Amesema kuwa chanzo cha mgogoro huo ni mpaka wa wilaya za Bunda, Serengeti na Butiama ambao unahusisha eneo la ekari 3,535 ambapo Wegesa Gikene na Nyamhanga Gembo wakazi wa Kijiji cha Remng'orori waliuawa kwa kukatwa na mapanga wakati wakiwa shambani.

Tuesday, 9 January 2018

Wananchi Bunda stoo walidhishwa na huduma ya umeme ya REA



Wananchi wa kata Bunda stoo katika halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara wameeleza namna wamenufaika na huduma ya umeme wa REA ikiwa ni pamoja na kijipatia maendeleo ya kiuchumi kutokana na huduma hiyo.
Hayo yamesemwana baadhi ya wananchi wa mashine ya maji na migungani wakati wakizungumza na mazingira hii leo wamesema huduma ya umeme wa REA umewafikia walengwa kwa gharama nafuu ya elfu ishirini na saba kuvuta umeme huo ambapo huduma hiyo imeanza mwaka jana .

Wameongeza kuwa wengi wao katika maeneo hayo wamenufaika na uhuduma hiyo na wanafaaidika kutokana na huduma hiyo kuwasaidia katika matumizi ya nyumbani ikiwemo mwanga na kuchaji simu pia wanajipatia uchumi kupitia huduma hiyo ikwa ni pamoja na miradi inayotegemea umeme huo kama kuchajisha simu kuwaingizia kipato.

Aidha wamemuomba diwani wa kata ya bunda stoo kutembelea wakazi wa maeneo hayo kuwasikiliza matatizo yao ikiwemo tatizo la maji ambapo limekuwa tatizo katika maeneo mbalimbali ya mji wabunda.

Maji safi na salama yamekuwa adimu kupatikana mtaa wa Migungani Halmashauri ya mji wa Bunda



Hali ya upatikanaji maji safi na salama katika mtaa wa Migungani kata ya Bunda stoo  halmashauri ya mji wa Bunda mkoa wa Mara hairidhishi kutokana na huduma hiyo kuwa hafifu katika eneo hilo.

Wakizungumza na mazingira fm kwa  nyakati tofauti  baadhi ya wakazi wa eneo hilo wamesema  hali ya upatikanaji wa maji inazidi kuwa ngumu kutokana na ukame unaokabili maeneo.

Stivine Warioba mkazi wa migungani amedai kuwa mamlaka ya maji katika halmashauri ya mji BAWASA, wamekataa uuzaji wa maji katika mabomba ya watu binafsi kutokana kutojaza mikataba ya awali ya kuuza maji .

Naye mwenyekiti wa mtaa wa migungani bwana Elias Robati amekiri kuwepo tatizo la maji na tayari linafaniwa ufumbuzi ikiwemo kukusanya michango mbalimbali kutoka kwa wananchi kuweza kusambaza line kubwa ya mabomb.

Aidha wananchi hao wameiomba halmashauri ya mji huo kutatua tatizo hilo haraka kwani imekuwa ni kero kwani  wanawake na watoto ndiyo wenye kupata adha hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Mara azungumzia matukio ya ukatili yanayoendelea kutokea Ndani ya Mkoa Wake.



Wito umetolewa kwa Jamii  ya Mkoa wa Mara kutakiwa kufanya kazi kwa ukaribu na viongozi wa serikali ili kuhakikisha kuwa vitendo wa ukatili wa kijinsia vinakomeshwa ndani ya mkoa huo.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Adam Malima wakati akizungumza katika uzinduzi wa saccos ya wanawake wa halmashauri ya mji wa Bunda siku ya leo katika viwanja vya ofisi ya halmashauri hiyo.

Malima amesema hivi karibuni ndani ya mkoa wa Mara kumetokea matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa watoto wa kike jambo ambalo sio la kuvumilikaa hata mara moja.

Aidha Malima amewasihi wa wanawake kuendelea na umoja walionao sasa ili wawe mfano hata kwa mikoa mingine katika kuelekea uchumi wa kati ndani ya nchi yetu.

Katika suala la uzinduzi wa SACCOS hiyo ofisi ya mkuu wa Mkoa imechangia Laki tano za kitanzania ili kuwawezesha wanawake hao katika kujikwamua kiuchumi.

Grace Marwa ambaye ni mbunge wa viti maalum mkoa wa Mara yeye katika nafasi yake amekabidhi hati ya kiwanja chenye thamani ya Milioni Nne huku akiahidi kama saccos hiyo itaendelea vizuri atatoa mshahara wake wa miezi miwili kuwawezesha wanawake hao kukuza saccos yao.

Naye Mkurungezi wa mji wa Bunda Janeth mayanja amewahakikishia wanawake hao kuwa halmashauri ya mji wa bunda itafanya kazi kwa ukaribuni na Saccos hiyo ambayo ina jumla ya wanachama 450 na kwamba halmashauri imechangia milioni kumi katika saccos hiyo.