← NYUMBANI
MAZINGIRA FM • BUNDA, MARA

Wasiliana Nasi

Kwa habari, matangazo, udhamini, ushirikiano na mawasiliano ya jumla.

SIMU+255 621 046 491 PIGA SIMU →
BARUA PEPEmazingirafm@gmail.com TUMA BARUA →
ANWANIP.O. Box 51, Saranga/Kabarimu

Bunda, Mara • 31530

MATANGAZO NA UDHAMINI

Fanya kazi na Mazingira FM

Kwa matangazo ya biashara, udhamini wa vipindi, kampeni za jamii na ushirikiano wa mawasiliano, wasiliana nasi kupitia simu au barua pepe.

TUFUATE

Mazingira FM Mitandaoni

Facebook Instagram YouTube X / Twitter
← NYUMBANI
MAZINGIRA FM • 91.7

Kuhusu Mazingira FM

Sauti ya Jamii — redio yenye maudhui ya kijamii kutoka Bunda, Mkoa wa Mara.

Wasifu wa Kituo

Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kituo kinarusha matangazo yake kutoka Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara pamoja na Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza kama Magu na Ukerewe.

Kupitia vipindi na matangazo yake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.

MTANDAO WETU

Vituo Vinne vya Matangazo

BUNDAKituo Kikuu
MUSOMAMara
TARIMEMara
MUGUMU–SERENGETIMara
SAUTI YA JAMII

Redio ya Jamii

Mazingira FM inalenga kuipa jamii nafasi ya kupata habari na maarifa, kusikiliza mijadala yenye manufaa, kushiriki katika masuala yanayoigusa na kupata burudani kupitia vipindi vinavyoakisi maisha ya jamii.

← NYUMBANI
MAZINGIRA TV

Video kutoka Mazingira FM

Tazama habari, mahojiano, matukio ya jamii na vipindi vya Mazingira FM.

MAZINGIRA FM • VIDEO

Mazingira TV

Video za habari na shughuli za jamii kutoka Bunda, Mara na maeneo yanayofikiwa na Mazingira FM.

FUNGUA YOUTUBE →
MAZINGIRA FM 91.7
Sauti ya Jamii • Mara, Tanzania
← NYUMBANI
MAZINGIRA FM NEWSROOM

HABARI

Habari na taarifa kutoka Mazingira FM.
Inapakia habari...
← RUDI HABARI MPYA
Inapakia habari...
● LIVEMazingira FM 91.7 MHzSikiliza Sasa — Sauti ya Jamii
HABARI MPYAMazingira FM • Sauti ya Jamii • Habari kutoka Mara

Mazingira FM — Sauti ya Jamii

Mazingira FM ni kituo cha redio chenye maudhui ya kijamii kilichoanzishwa mwaka 2011. Kinarusha matangazo yake kutoka Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara, na kusikika katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mara, Mkoa wa Simiyu na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Mwanza, ikiwemo Magu na Ukerewe. Kupitia vipindi vyake, Mazingira FM hutoa habari, elimu, mazingira, afya, michezo na burudani kwa jamii.

♫ Sikiliza Live

Mazingira FM 91.7 MHz

Bonyeza Play kusikiliza matangazo
Mtandao wetu

Vituo 4 vya Matangazo

BundaMain Site
MusomaTransmission Site
TarimeTransmission Site
MugumuSerengeti
Newsroom

Habari Mpya

Machapisho mapya kutoka Mazingira FM.

HABARI ZA SASA
Inapakia habari mpya kutoka Mazingira FM...
HABARI ZAIDIHabari kutoka kwenye kumbukumbu za Mazingira FM

Tuesday, 22 April 2025

Radio jamii zanolewa kumulika nafasi ya wanawake uchaguzi mkuu 2025

 

Picha ya pamoja washiriki wa mafunzo kwa radio jamii Tanzania yaliyotolewa na TAMWA kwa kushirikiana na TADIO jijiji Dodoma

Licha ya sensa ya watu na makazi ya 2022 kuonesha idadi ya wanawake ni wengi kuliko wanaume, katika nafasi za uongozi kwa ngazi za udiwani na ubunge bado kuna idadi ndogo zaidi ya uwakilishi.

By Edward Lucas

Chama cha Wanahabari Wanawake Tanzania TAMWA kwa kushirikiana na TADIO wameendesha mafunzo kwa radio za kijamii Tanzania Bara kuandaa habari na vipindi vitakavyowawezesha wanawake kushiriki kikamilifu hasa kwa kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2025.

Akizungumzia mafunzo hayo, Meneja Mipango na Mikakati TAMWA, Sylivia Daulinge amesema mafunzo hayo yanayodhaminiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Vyombo vya Habari Finland VIKES yamelenga elimu ya namna bora ya kuandaa vipindi vya usawa na ujumuishi wa masuala ya kijinsia kwa kuhakikisha wanawake hasa vijana na makundi maalumu yanapewa kipaumbele kuelekea uchaguzi mkuu.

Sylivia Daulinge, Meneja Mipango na Mikakati TAMWA
Sylivia Daulinge, Meneja Mipango na Mikakati TAMWA

Kwa upande wake Mkufunzi wa mafunzo hayo kutoka Radio Tadio, Hilali Alexander Ruhundwa amesema kwa kushirikiana na TAMWA wameona wanajukumu la kufanya katika jamii kwa kuwashirikisha waandishi wa habari ili kufikisha elimu kwa jamii kuwafanya wanawake washiriki kikamilifu katika uchaguzi ujao

Hilali Alexander Ruhundwa, Mkufunzi wa mafunzo kutoka Radio Tadio akieleza kuhusu malengo ya mafunzo kwa radio za jamii kuelekea uchaguzi wa 2025
Sauti ya Hilali Alexander Ruhundwa

Kwa takwimu za uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020, madiwani wanawake waliochaguliwa kwenye kata ni 260 kati ya 3,953 ambao ni sawa na asilimia 6.58 na kwa upande wa ubunge kati ya majimbo 264 wabunge wanawake waliochaguliwa kwenye majimbo ni 26 tu sawa na asilimia 9.85

No comments:

Post a Comment

Chagua Unachotaka Kusoma

Mazingira FM Newsroom
HabariHabari za Bunda, Mara, Tanzania na jamii tunayohudumia. MichezoMatokeo, ligi, vipaji na habari za michezo. MazingiraUhifadhi, hali ya mazingira, kilimo na maendeleo. JamiiAfya, elimu, wanawake, vijana na maendeleo ya jamii. KimataifaHabari za dunia na matukio ya kimataifa. SiasaHabari za siasa na uongozi. BurudaniSanaa, muziki na burudani. ElimuHabari zinazohusu elimu. UchumiBiashara, ajira, uchumi na maendeleo ya jamii.
Tufuate

Mazingira FM Mitandaoni

+255 621 046 491 • mazingirafm@gmail.com