Changamoto ya kukosa huduma ya Afya yawaibua wakazi wa mtaa wa Mine kata ya Kabasa-Bunda. - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 18 May 2023

Changamoto ya kukosa huduma ya Afya yawaibua wakazi wa mtaa wa Mine kata ya Kabasa-Bunda.

 

Zahanati inayojengwa mtaa wa Mine kata ya Kabasa-Bunda kwa nguvu za Wananchi

Wananchi wa mtaa wa Mine Kata ya Kabasa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wameungana pamoja katika shughuli ya maendeleo kwa kujenga Zahati ili kuondokana na changamoto ya huduma ya afya katika eneo hilo.
Mafundi wakiwa 'site' kazi ya ujenzi wa Zahanati inaendelea


Mwenyekiti wa kamati ya ujenzi wa zahanati hiyo, Samson Machibya amesema ni wiki ya pili hadi sasa tangu waanze ujenzi na wamefikia hatua ya 'lenta' ambapo katika hatua hiyo wananchi wamekuwa wakichangia fedha na kuleta mahitaji mbalimbali kama mawe, mchanga, kokoto na maji.

Samson Machibya, Mwenyekiti kamati ya Ujenzi wa Zahanati mtaa wa Mine 


Mhasibu wa kamati ya Ujenzi wa Zahanati, Lucas Budigila amesema katika hatua ya kujenga msingi wananchi walikubaliana kuchanga shilingi 13,500 na hatua za kuinua jengo walikubaliana kuchanga shilingi 32,000 kwa kila kaya ambazo zinauwezo wa kuchangia hii ni baada ya vikao na mapitio kwa kaya zenye uwezo na zisizo na uwezo.

Mhasibu wa kamati ya Ujenzi wa Zahanati mtaa wa Mine, Lucas Budigila Mwenyekiti wa Mtaa wa Mine, Shabani Juma Nkomba akiwa katika eneo la mradi kuhakikisha kazi ya wananchi inasimamiwa na nia ya kupata Zahanati inatimia.Songoma Ramadhani Omari ambaye ni mkazi wa mtaa huo amesema "mimi ni mwenyekiti wa Chadema lakini baada ya Uchaguzi maisha yanaendelea siwezi kupinga maendeleo wakina mama walivyokuwa wanahangaika, watu walikuwa wanafia njiani kwa ajili ya kupelekwa katika huduma za kujifungua ..."


Nao baadhi ya wanawake na akina mama wa mtaa huo wameupongeza mpango huo na kusema utawaondolea changamoto ya kutembea mwendo mrefu na watoto katika huduma ambazo zinaweza kupatikana pindi Zahanati itakapo kamilika.

No comments:

Post a Comment