AHADI YA KAMBARAGE IMEANZA KUTEKELEZWA KUPAUA OFISI YA CCM MCHARO-BUNDA - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Friday 5 May 2023

AHADI YA KAMBARAGE IMEANZA KUTEKELEZWA KUPAUA OFISI YA CCM MCHARO-BUNDA

Zoezi la upauaji jengo la ofisi ya CCM kata ya Mcharo lililopo mtaa wa Changuge-Bunda

Ikiwa ni wiki moja tangu Mwenyekiti wa kamati ndogo ya Fedha, Uchumi na Mipango CCM Wilaya ya Bunda, Kambarage Wasira afike kata ya Mcharo kuunga mkono juhudi za ujenzi wa ofisi ya CCM tayari kazi ya upauaji imeanza leo tarehe 5 May 2023.


Akizungumza na Radio Mazingira FM wakati wa zoezi la upauaji wa jengo hilo Mwenyekiti wa CCM kata ya Mcharo, Phinias Kasoga Budeba amesema baada ya kupokea mabati kutoka kwa Kambarage Wasira siku ya jumatano tarehe 3 May 2023 alipokea mbao na vifaa vingine vilivyokuwa vimeahidiwa hivyo kwa sasa wanaendelea na kazi.


"Baada ya jana kukutana tulipata taarifa kutoka kwa katibu kwamba tayari sasa kesho mafundi wanafika na shughuli ikaanzishwa, mpaka sasa kweli tuko hapa mafundi wako juu shughuli inaendelea kuchapwa kikamilifu sana" amesema Phinias Kasoga.

Mwenyekiti wa CCM kata ya Mcharo, Phinias Kasoga Budeba akiendelea kushuhudia hatua ya upauaji wa ofisi inayojengwa mtaa wa Changuge-Bunda


Naye Katibu wa CCM kata ya Mcharo, Samwel Makindi amesema  jengo hilo lina jumla ya vyumba vitatu(3) vya ofisi kwa ajili ya viongozi mbalimbali na ukumbi wa mikutano. Hivyo amewashukuru wadau wote waliotoa michango yao katika kufanikisha ujenzi wa jengo hilo na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuchangia ili kukamilisha ujenzi wa ofisi hiyo kwani bado litahitajika kuwa na madirisha, milango, rangi na vitu vingine.

Katibu wa CCM kata ya Mcharo-Bunda, Samwel Makindi akiwa katika viwanja vya jengo la ofisi ya CCM mtaa wa Changuge akishuhudia kazi inavyoendelea.Jengo la ofisi ya CCM kata ya Mcharo lenye vyumba vitatu vya ofisi na ukumbi wa mikutano  likiendelea kuezekwa leo tarehe 5 May 2023


No comments:

Post a Comment