Saturday, 29 April 2023

'KAMBARAGE WASIRA AWAUNGA MKONO CCM KATA YA MCHARO'

 



Mwenyekiti wa kamati ndogo ya fedha, uchumi na mipango ccm wilaya ya Bunda, Kambarage Masatu Wasira amechangia mabati 64 yenye thamani ya shilingi mil 1.7 kwa ajili ya uendelezaji na ukamilishaji wa ujenzi ofisi ya ccm kata ya Mcharo. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi mabati hayo jana tarehe 28 April 2023 amesema katika kata hiyo kuna changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi wa ofisi ya ccm ambayo ina takribani miaka 4 tangu kuanza ujenzi huo lakini mpaka sasa bado haujakamilika.

"Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mh Chandi Marwa aliwaahidi kuwapa shilingi laki 5 lakini pia kwa ujio wetu huu tumeweza kupata wadau pia wamechangia zaidi ya laki 5 ya kusaidia misumali na vitu vingine ili shughuli iendelee na mbao zitaingia siku ya jumatatu kutoka kwa Kazi mfanyabiashara wa Mwanza ambaye naye amejitoa kuchangia" amesema Kambarage Wasira.



Kambarage Masatu Wasira akikabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi ofisi ya ccm kata ya mcharo

Kwa upande wake Mwenyekiti CCM kata ya Mcharo, Ndugu Phinias Kasoga amesema kutokana na ukosefu wa ofisi wamekuwa na mazingira magumu katika utekelezaji wa majukumu yao mfano utunzaji wa nyaraka za chama na kwamba kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza ufasi wa kazi.

"Tumekuwa na mazingira magumu kidogo kwasababu ofisi ambayo tumekuwa tukiitumia katika masuala yetu ni ofisi ya tawi ambapo unakuta ofisi moja imebeba mamlaka nyingi wakati mwingine amani ilikuwa haikai vizuri au utunzaji wa kumbukumbu za kichama umekuwa na changamoto sana" amesema Phinias Kasoga. 



Picha ya Jengo la ofisi za CCM kata ya Mcharo lililopo mtaa wa Changuge ambalo linawekewa mipango ya kukamirishwa


Mabati 'bando 4' yaliyotolewa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya fedha, uchumi na mipango CCM wilaya ya Bunda, Kambarage Masatu Wasira yakikabidhiwa kwa uongozi wa CCM kata ya Mcharo.





Baadhi ya wanachama na viongozi wa CCM kata ya Mcharo wakiwa katika mazungumzo kabla ya zoezi la kukabidhi mabati lilolofanyika katika eneo la Changuge


Tuesday, 25 April 2023

BUNDA KINARA WIZI KWENYE MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MARA.

 

RC MARA, MEJA JENERALI SULEIMANI MZEE

Imeelezwa kua katika miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali mkoani Mara Wilaya ya Bunda inaongoza kwa wizi wa vifaa vya ujenzi  wa miradi  hiyo jambo ambalo linarudisha nyuma juhudi za serikali.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Mkoa wa Mara  Meja jenerali Sulemani Mzee katika ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa chujio la maji  Nyabehu  wenye gharama ya zaidi ya Tsh.  bilioni 10 na ambao utanufaisha wakazi wote wa wilaya Bunda pindi utakapo kamilika.

Akiwa katika eneo la mradi huo RC Mzee amesema suala la wizi katika miradi ya serikali linasikitisha hasa wilaya ya Bunda na kuwataka wananchi kuwa walinzi wa miradi hiyo.


Hata hivyo mkuu wa mkoa amewapongeza  BUWSSA kwa kazi nzuri ambayo wanaendelea kuifanya katika kutekeleza mradi huo huku akiwata wasimamizi kurekebisha sehemu zenye kasoro ili kuendana na thamani ya pesa inayotolewa naserikali.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Dr. Vicent Naano amemshukuru mh. Rais Samia Suluhu Hassan  kwa kuwezesha ujenzi wa chujio hilo huku akiwataka BUWSSA kuweka mfumo wa kisasa wa ulinzi utakao saidia kudhibiti uharibifu wa mradi huo.



Awali akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji  safi na usafi wa mazingira Bunda BUWSSA Ester Gilyoma amesema utekelzaji wa mradi huo umefikia asilimia 99 na sasa wananchi wanapata maji safi na salama tofauti na ilivyo kua awali.

Saturday, 22 April 2023

WAKAAZI WA TAMAU WAOMBA UONGOZI WA WILAYA YA BUNDA KUFIKA MARA KWA MARA ILI KUSIKILIZA KERO ZAO KATIKA MCHAKATO WA KUHAMISHWA

 

Wananchi wa mtaa wa Tamau kata ya Nyatwali wakiwa katika mkutano kujadili hatima yao katika eneo hilo.


Wananchi wa Mtaa wa Tamau kata ya Nyatwali Halmashauri ya Mji wa Bunda Mkoani Mara wameuomba uongozi wa Wilaya hiyo kufanya mikutano ya mara kwa mara katika maeneo yao ili kuwawezesha kupata taarifa na ufafanuzi wa baadhi ya mambo yanayohusu mchakato wa kuhamishwa katika eneo hilo.


Wakizungumza katika mkutano wa hadhara ulioitishwa na uongozi wa mtaa huo eneo la shule ya msingi Tamau jana tarehe 21 April 2023 wenye lengo la kuelimisha wananchi kufungua akaunti za benki na kuwapa taarifa juu ya utaratibu uliotolewa kwa wale wenye malalamiko mbalimbali, wananchi hao wamesema ni vema uongozi wa Wilaya ukawa na utaratibu wa kufika ili kuwasikiliza kama ilivyokuwa sehemu ya ahadi zao.




Mkaazi wa Tamau akichangia mawazo yake katika mkutano wa wananchi na viongozi wa mtaa huo.





Katika mkutano huo wananchi hao wamekuwa na hoja mbalimbali ikiwa ni pamoja na mchakato wa utathimini wa maeneo yao, kiwango cha fedha kinachopendekezwa, mchakato wa ufunguzi wa akaunti na mambo mengine ambayo bado wanaona licha ya majibu yanayotolewa kupitia uongozi wa mtaa huo bado wanaona kuna umuhimu kwa uongozi wa ngazi za juu kufika mara kwa mara ili kuwasikiliza.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa mtaa huo, Asafu Ernest Owiti amesema mtathimini mkuu wa taifa ameunda kamati inayoongozwa na Diwani wa kata hiyo huku katibu wake akiwa ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda ili kufuatilia malalamiko mbalimbali ya wananchi kisha kutoa mapendekezo ambayo yatawasilishwa kwa mtathimini kwa hatua zaidi.


Mwenyekiti wa Mtaa wa Tamau, Asafu Ernest Owiti


Naye Afisa Mtendaji Mtaa wa Tamau, Dotto Mirumbe amesema katika mkutano walialika benki mbalimbali kufika ili kutoa elimu na maelekezo ya namna ya kufungua akaunti lakini wote wameshindwa kufika kutokana na sababu mbalimbali hivyo zoezi hilo litafanyika siku ya jumatatu tarehe 24 April 2023 hii ikiwa ni moja kati ya hatua ya kutoa ufumbuzi kwa baadhi ya maswali inayoibuka kwa wananchi hao.

Dotto Kihiri Mirumbe, Afisa Mtendaji Mtaa wa Tamau akitoa ufafanuzi wa baadhi ya hoja kwa wananchi wa Tamau.


Baadhi ya wananchi wakiwa wanafuatilia mkutano wakiwa nje baada ya chumba cha darasa kukosa nafasi













Sunday, 16 April 2023

Baba amlawiti mwanaye ili kuinua huduma yake ya M-pesa kijiji cha Mwibagi Wilaya ya Butiama

 

Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Pascal Sanga

Baba amlawiti mwanaye ili kuinua huduma yake ya M-pesa huku wengine wakifanya vitendo vya ubakaji kwa imani za kishirikina kwa lengo la kupata dhahabu katika machimbo.


Hayo yamebainishwa na Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Pascal Sanga wakati wa Kongamano la kuadhimisha siku ya kuzaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere lililofanyika katika viwanja vya Kituo cha Makumbusho ya Mwl Nyerere Butiama Mkoani Mara tarehe 15 April 2023.


Akiwasilisha mada kuelezea uzoefu wa kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto katika Wilaya hiyo, Sanga amesema licha ya mafanikio mbalimbali katika juhudi za kukabiliana na vitendo vya ukatili kumekuwa na mila na destori potofu katika imani za kishirikina zinazochangia kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani humo.https://www.instagram.com/p/CrF0FXIOFuM/






















Saturday, 15 April 2023

Kongamano kuadhimisha kuzaliwa Hayati Mwl Nyerere limefanyika leo Butiama


Makumbusho ya Taifa kupitia kituo cha Makumbusho ya Mwl Nyerere kilichopo Butiama Mkoani Mara, leo tarehe 15 April 2023 kimefanya Kongamano katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere tarehe 13 April 1922.

Katika Kongamano hilo lililowahusisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kutokana maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara liliongozwa na mada kuu katika tafakuri ya mchango wa Mwl Nyerere kutetea na kulinda haki za wanawake na watoto.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama, Emmanuel Kiondo amesema wamefanya maadhimisho hayo ili kupata nafasi ya kujadiliana kuhusu baba wa Taifa alizungumza nini na kama Makumbusho ya Taifa wajibu wao ni kulikumbusha taifa na jamii juu ya mitizamo na falsafa za Hayati Baba wa Taifa.


Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama, Emmanuel Kiondo 

Kiongozi wa kabila la Wazanaki kutoka ukoo wa Mwl Nyerere, Chief Japhet Wanzagi 
akizungumza katika kongamano kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa hayati Mwl Nyerere kueleza nafasi ya Mila na Desturi katika kutetea haki za wanawake na watoto na msimamo



Mkurugenzi-Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Pristiana Samwelly akiwasilisha mada ya mchango wa taasisi zisizo za kiserikali katika kutetea haki za wanawake na watoto.



Mwenyekiti wa Kongamano kumbukizi ya kuzaliwa Mwl Nyerere, Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  akiongoza zoezi.





Levina Julius Marwa, Afisa Tarafa ya Kiagata aliyekuwa mgeni rasmi akiwakilisha ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama akieleza juhudi zinazofanywa na Wilaya hiyo katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.



Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Pascal Sanga akiiwakilisha ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Butiama kueleza uzoefu wa kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto katika Wilaya hiyo.


Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi, Edwin Lyimo akieleza uzoefu wa Jeshi la Polisi katika kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto mkoani Mara.



Washiriki wa Kongamano katika viwanja vya Makumbusho ya Mwl Nyerere Butiama wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali  huku baadhi wakichangia katika mjadala.






Aidha katika Kongamono hilo iliandaliwa pia keki maalumu kutoka Kituo cha Mkaumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama kwa ajili ya washiriki hususani watoto.




























Friday, 14 April 2023

Wazazi waaswa kuwalea watoto katika maadili mazuri ili kuepukanana na masuala ya ushoga

ikiwa tarehe 13 mwezi wa 4 kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Baba wa Taifa la Tanzania Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Wazazi Wametakiwa Kuwalea Watoto Katika Maadili Mazuri  ili Kuepukana Na jamii isiyofaa. 

 Hayo yamesemwa katika ufunguzi wa wiki ya kuzienzi falsafa za baba wa taifa ulioandaliwa na taasisi ya Mwl Nyerere Faundation iliyofanyika wilayani Butiama mkoani Mara na kuudhuriwa naviongozi mbalimbali. 

 Akizungumza katika kongamano hilo la ufunguzi mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dr  Vicent Anney Naano amesema kazi kubwa ya baba wa taifa aliyoifanya kwa taifa la Tanzania haiwezi kusahaurika akizungumzia suala la kuondoa ukabila miongoni mwa watanzania. 


 Naye mwenyekiti wa bodi ya wadhamini ya taasisi ya Mwalimu Nyerere Faundation Joseph Warioba Butiku amesema mkoa wa Mara ndiyo uliomzaa Baba wa Taifa ambapo misingi ya kiongozi huyo ilikuwa ni utu, usawa na haki na ndivyo vilivyoleta amani na kama watu wa Mara hawaviamini wanaamini nini?. 


 Naye mgeni rasmi ambaye ni mbunge wa jimbo la Butiama ambaye pia ni naibu waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe Jumanne Sagini amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hasani imeendelea kuzienzi falsafa za baba wa taifa kwa kutekeleza miradi ambayo ilikuwa ndoto ya baba wa taifa kama vile bwawa la kufua umeme la mwalimu nyerere, serikali kuamia Dodoma, ujenzi wa hospitali ya kwangwa musoma na ukamilishwaji wa barabara ya makutano sanzate kwa kiwango cha lami.


 Aidha ameongeza kuwa ni jukumu la wazazi na walezi kwenye jamii kuwalea watoto katika maadili Mazuri kwa ajili ya kizazi kijacho na kuwaepusha na mambo mabaya ikiwemo ndoa za jinsia moja na masuala ya ushoga huku akisema serikali itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watakaodhibitika kujihusisha na masuala ya ushoga.