Mwenyekiti wa kamati ndogo ya fedha, uchumi na mipango ccm wilaya ya Bunda, Kambarage Masatu Wasira amechangia mabati 64 yenye thamani ya shilingi mil 1.7 kwa ajili ya uendelezaji na ukamilishaji wa ujenzi ofisi ya ccm kata ya Mcharo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mabati hayo jana tarehe 28 April 2023 amesema katika kata hiyo kuna changamoto ya upatikanaji wa vifaa vya ujenzi wa ofisi ya ccm ambayo ina takribani miaka 4 tangu kuanza ujenzi huo lakini mpaka sasa bado haujakamilika.
"Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mh Chandi Marwa aliwaahidi kuwapa shilingi laki 5 lakini pia kwa ujio wetu huu tumeweza kupata wadau pia wamechangia zaidi ya laki 5 ya kusaidia misumali na vitu vingine ili shughuli iendelee na mbao zitaingia siku ya jumatatu kutoka kwa Kazi mfanyabiashara wa Mwanza ambaye naye amejitoa kuchangia" amesema Kambarage Wasira.
Kambarage Masatu Wasira akikabidhi mabati kwa ajili ya ujenzi ofisi ya ccm kata ya mcharo
Kwa upande wake Mwenyekiti CCM kata ya Mcharo, Ndugu Phinias Kasoga amesema kutokana na ukosefu wa ofisi wamekuwa na mazingira magumu katika utekelezaji wa majukumu yao mfano utunzaji wa nyaraka za chama na kwamba kukamilika kwa jengo hilo kutaongeza ufasi wa kazi.
Mabati 'bando 4' yaliyotolewa na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya fedha, uchumi na mipango CCM wilaya ya Bunda, Kambarage Masatu Wasira yakikabidhiwa kwa uongozi wa CCM kata ya Mcharo.
No comments:
Post a Comment