Kongamano kuadhimisha kuzaliwa Hayati Mwl Nyerere limefanyika leo Butiama - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Saturday 15 April 2023

Kongamano kuadhimisha kuzaliwa Hayati Mwl Nyerere limefanyika leo Butiama


Makumbusho ya Taifa kupitia kituo cha Makumbusho ya Mwl Nyerere kilichopo Butiama Mkoani Mara, leo tarehe 15 April 2023 kimefanya Kongamano katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa Hayati Baba wa Taifa Mwl Nyerere tarehe 13 April 1922.

Katika Kongamano hilo lililowahusisha wadau mbalimbali ikiwa ni pamoja na walimu, wanafunzi wa shule za msingi, sekondari na vyuo kutokana maeneo mbalimbali ya mkoa wa Mara liliongozwa na mada kuu katika tafakuri ya mchango wa Mwl Nyerere kutetea na kulinda haki za wanawake na watoto.

Akizungumza katika ufunguzi wa Kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama, Emmanuel Kiondo amesema wamefanya maadhimisho hayo ili kupata nafasi ya kujadiliana kuhusu baba wa Taifa alizungumza nini na kama Makumbusho ya Taifa wajibu wao ni kulikumbusha taifa na jamii juu ya mitizamo na falsafa za Hayati Baba wa Taifa.


Mkurugenzi Mkuu wa Makumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama, Emmanuel Kiondo 

Kiongozi wa kabila la Wazanaki kutoka ukoo wa Mwl Nyerere, Chief Japhet Wanzagi 
akizungumza katika kongamano kuadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa hayati Mwl Nyerere kueleza nafasi ya Mila na Desturi katika kutetea haki za wanawake na watoto na msimamo



Mkurugenzi-Hope for Girls and Women Tanzania, Rhobi Pristiana Samwelly akiwasilisha mada ya mchango wa taasisi zisizo za kiserikali katika kutetea haki za wanawake na watoto.



Mwenyekiti wa Kongamano kumbukizi ya kuzaliwa Mwl Nyerere, Makamu Mkuu wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere  akiongoza zoezi.





Levina Julius Marwa, Afisa Tarafa ya Kiagata aliyekuwa mgeni rasmi akiwakilisha ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama akieleza juhudi zinazofanywa na Wilaya hiyo katika kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia.



Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Butiama, Atula Pascal Sanga akiiwakilisha ofisi ya Mkurugenzi Wilaya ya Butiama kueleza uzoefu wa kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto katika Wilaya hiyo.


Mkaguzi Msaidizi Jeshi la Polisi, Edwin Lyimo akieleza uzoefu wa Jeshi la Polisi katika kulinda na kutetea haki za wanawake na watoto mkoani Mara.



Washiriki wa Kongamano katika viwanja vya Makumbusho ya Mwl Nyerere Butiama wakiendelea kufuatilia mada mbalimbali  huku baadhi wakichangia katika mjadala.






Aidha katika Kongamono hilo iliandaliwa pia keki maalumu kutoka Kituo cha Mkaumbusho ya Mwl Nyerere-Butiama kwa ajili ya washiriki hususani watoto.




























No comments:

Post a Comment