Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amejibu tuhuma
za mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema, na kumtaka asipotoshe wananchi,
bali apeleke malalamiko yake kwenye kamati.
Spika
Ndugai ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akiendesha bunge, na kusema
kwamba bunge lina utaratibu wake kwenye kila jambo linalohusika bungeni
hapo.
"Lema
asipotoshe wananchi aende hadharani kwenye kamati kuzungumzia hayo,
bunge haliwezi kusimama kwa shambulio la Lissu bali kanuni zinasema
mbunge akifariki bunge linasimama kwa siku moja. Na iwapo Spika
akiletewa jambo la maadili linapelekwa kamati ya maadili, suala la jinai
linapelekwa polisi", amesema Spika Ndugai
Pia
Spika Ndugai amesema suala la Tundu Lissu kuchangiwa fedha za matibabu
na wabunge wakati yeye alitibiwa nje ya nchi ni kwamba matibabu ya Tundu
Lissu yameenda kinyume na utaratibu wa bunge.
"Wabunge
wanaopelekwa nje (India) wanapewa rufaa kutoka hospital ya Muhimbili
lakini si kama alivyopelekwa Lissu", amesema Spika Ndugai.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amesema anamsamehe Godbless Lema na kuwataka watu kumsamehe kwani hajui alitendalo.
Hapo
jana mbunge wa Arusha Godbless Lema alimlaumu Spika Ndugai kuwa
anashindwa kutetea kiti chake, kwa kuzidi kuwakandamiza wabunge wa
upinzani hususan suala la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu.
No comments:
Post a Comment