Tuesday, 18 July 2023

Bunda: Vifo vya kusikitisha watoto wawili wa familia moja, msichana wa miaka 18 ashukiwa kuhusika

Shimo la Choo alimokutwa mtoto Evans Martin (2). Picha na Edward Lucas

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia katika matukio tofauti huku mwingine wa miaka miwili akinusurika kifo baada ya kuopolewa kwenye shimo la choo, msichana wa miaka 18 ambaye ana muda wa takribani miezi miwili tangu afike kwenye hiyo familia ashukiwa kuhusika

Na Edward Lucas

Watoto wawili wa familia moja wamefariki dunia katika matukio tofauti huku mmoja akinusurika kifo baada ya kutumbukia kwenye shimo la choo mtaa wa Nyamatoke kata ya Mcharo Wilaya ya Bunda Mkoani Mara.

Tukio la kwanza lilitokea tarehe 5 July 2023 majira ya saa 11 jioni mtoto Evalin Martin(10) alikufa maji kwa kutumbukia kwenye mkondo wa mto Rubana wakati alipokwenda kuchota maji wakiwa wameambatana na msichana aliyetambulika kwa jina la Helena ambaye ni mtoto wa shangazi yake.

Akisimulia tukio hilo Neema Maduhu Gedi (47) ambaye ni mama wa Evalin amesema masaa machache baada ya mwanaye kuelekea mtoni akiwa na Helana alipokea taarifa ya mwanaye kuzama kwenye maji ambapo juhudi za kumtafuta zilifanikiwa kuupata mwili wake akiwa amepoteza maisha kabla ya siku chache baadaye mtoto wa mke mwenzake Evans Martin (2) kukutwa ndani ya shimo la choo masaa machache baada ya Helena kumpeleka kujisaidia.

Sauti ya Neema Maduhu Gedi (47) ambaye ni mama wa marehemu Evalin (10) akisimulia kifo cha mmwanaye na mtoto wa mke mwenziye alivyonusurika kwenye choo

Ikiwa bado familia inatafakari tukio la mtoto kutumbukia chooni, siku hiyo hiyo tarehe 12 July 2023 mida ya saa 11 jioni Julius Martin (6) alipotea nyumbani ambapo juhudi za kumtafuta kutoka kwa familia na wananchi wengine waliokutanishwa kwa njia ya yowe hazikuweza kuzaa matunda hadi mida ya usiku walipoazimia kwenda kupumzika.

Kesho yake zoezi la kutafuta liliendelea na mida ya saa 5:00 asubuhi walifanikiwa kuupata mwili wa mtoto huyo kando kando ya mlima ulio umbali wa mita 400 toka nyumbani kwao katika zoezi lililofanikishwa kwa asilimia kubwa na Helena jambo lililoongeza mashaka zaidi juu ya mgeni wao huyo waliyempokea tangu tarehe 27 Mei 2023 akitokea nchini Kenya kwa mama yake.

Ester Constantine Lukonge, Mama wa mtoto Evans aliyetumbukia chooni na Julius aliyekutwa amefariki mlimani akisimulia tukio

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyamatoke, Sangi Mago Mahemba amesimulia mashaka waliyopata wananchi kuhusu maelezo ya Heleni juu ya namna alivyobaini mwili huo ambapo hatimaye jeshi la polisi liliondoka naye kwa uchunguzi zaidi.

Mwenyekiti mtaa wa Nyamatoke, Sangi Mago Mahemba akisimulia namna mwili wa mtoto Julius ulivyopatikana

Mazingira Fm amemtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salum Ramadhani Morcase ambaye amethibitisha kutokea tukio hilo

Sauti ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mara, ACP Salum Ramadhani Morcase kuhusiana na tukio hilo



Ujenzi wa Shule Shikizi Kihumbu wa milioni 348.5 utakamilika 30 July 2023, Mbunge Getere autembelea

 

Mbunge Mwita Getere akiwa katika moja ya vyumba vya madarasa ya shule shikizi Kihumbu akiangalia utekelezaji

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Shule hiyo, Gatida Maregesi ambaye ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kihumbu amesema mradi huo uliopo eneo kitongoji cha Sabasita uko chini ya shule ya Msingi Kihumbu kata ya Hunyari jimbo la Bunda ambao ulipokea kiasi cha shilingi milioni 348.5 kupitia mradi wa 'BOOST'

Amesema fedha ya mradi huo iliingia tarehe 21 April 2023 ambapo utekelezaji wa mradi huo kupitia 'Force Account' ulianza tarehe 19 Mei 2023 na ulitarajiwa kukamilika tarehe 30 June 2023 lakini baadaye muda uliongezwa hadi tarehe 30 July 2023 ndipo unatarajiwa kukamilika.







Gatida amesema vyumba tisa (9) vya madarasa vimeshaezekwa na sasa wako katika hatua ya 'kuskimu', vyoo matundu 8 vimekamilika na kuezekwa, jengo la utawala linakamilika kupigwa 'lipu' na hivyo kufikia tarehe 30 July 2023 mradi utakuwa umekamilika na kukabidhiwa.







Sunday, 16 July 2023

BAVICHA kuadhimisha siku ya vijana duniani mkoani Mwanza

Zacharia Mbubura Ramadhani katibu wa BAVICHA Bunda mjini, Picha na Adelinus Banenwa

BAVICHA maadhimisho ya siku ya vijana Duniani yatafanyiaka Mwanza kauli mbiu kijana ijue na itambue nguvu yako, lengo ni kuwakutanisha vijana na badarishana mawaza ya fursa zilizopo.

Na Adelinus Banenwa

Baraza la vijana  chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA wanatarajia kuadhimisha siku ya vijana duniani jijini Mwanza huku kauli mbiu ikiwa ni “kijana ijue na itambue nguvu yako”.

Hayo yamesemwa na katibu wa baraza la vijana BAVICHA jimbo la Bunda mjini Zacharia Mbubura Ramadhani wakati akizungumza na mazingira fm ambapo amewataka vijana wa chama hicho kuhakikisha wanafika katika maadhimisho hayo kwa kuwa kuna fursa nyingi zinaweza kujitokeza.

Zacharia Mbubura Ramadhani katibu wa BAVICHA Bunda mjini

Akizungumzia suala la vijana kukataa kujihusisha na siasa Zacharia amesema siasa ni maisha hivyo kila mtu analazimika kuingia katika mfumo huo kwa kuwa kila jambo linalofanyika linategemea maamuzi ya wanasiasa.

Zacharia Mbubura Ramadhani katibu wa BAVICHA Bunda mjini

Ikimbukwe kwamba siku ya vijana duniani huadhimishwa kiala tarehe 12 mwezi  wa nane kila mwaka ikiwa Madhumuni ya siku hiyo ni kuelekeza umakini kwenye masuala ya kitamaduni na kisheria yanayowazunguka vijana amabapo maadhimisho ya kwanza yalifanyika mwaka 2000.

Masaburi: urasimu chanzo kusitishwa mikopo ya halmashauri

 

Mhe Juliana Didas Masaburi mbunge viti maalumu CCM kupitia kundi la vijana, Picha na Adelinus Banenwa

Urasimu chanzo cha kusitishwa kwa mikopo ya asilimia kumi kutoka mapato ya ndani ya halmashauri ambapo serikali inaandaa mfumo mwwingine ambao makundi ya akina mama vija na wenye ulemavu watatumia kupata fedha hizo.

Na Adelinus Banenwa

Imeelezwa kuwa serikali imeamua kubadirisha mfumo wa kukopesha vikundi katika mpango wa asilimia kumi kutoka mapato ya ndani ya halmashauri nchini kutokana na urasimu uliyokuwa unatumika katika mikopo hiyo.

Hayo yamesemwa na mbunge viti maalumu CCM kupitia kundi la vijana Mhe Juliana Didas Masaburi katika baraza lililoandaliwa na Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Bunda ambapo pamoja na mambo mengine alifika kusikiliza kero za vijana na changamoto ndani ya jumuiya hiyo.

Mhe Masaburi amesema kutokana na changamoto hiyo ya urasimu serikali imelazimika kubadirisha mfumo baada ya wabunge kuishauri hivyo kuanzia dirisha litakapofunguliwa la mikopo hiyo ya asilimia 10 haitakuwa lazima kikundi bali hata mtu mmoja ataweza kukopeshwa ili mradi ajulikane anakwenda kufanya nini.

Mhe Juliana Didas Masaburi mbunge viti maalumu CCM kupitia kundi la vijana

Saturday, 15 July 2023

Mhe Masaburi, vijana Mara changamkia fursa

 

Mbunge wa viti maalumu kutoka kundi la vijana Mhe Juliana Didas Masaburi akisaini katika kitabu cha wageni katika baraza la UVCCM wilaya aya Bunda, Picha na Adelinus Banenwa

Ili kuhakikisha vijana wanaendelea kujikwamua kimaisha wametakiwa kuchanagmkia fursa zinazotolewa na serikali ikiwa ni pamoja na kuomba mikopo ya asilimia kumi kutoka halmashauri.

Na Adelinus Banenwa

Wito umetolewa kwa vijana mkoani Mara kuchangamkia fursa zinazotolewa na serikali ili kujikwamua kimaisha na kuondokana na utegemezi.
Wito huo umetolewa leo na Mbunge viti maalumu kupitia kundi la vijana Mhe Juliana Didas Masaburi katika baraza la Umoja wa vijana chama cha mapinduzi CCM lililofanyika ukumbi wa Helieth Bunda mjini
Mhe Masaburi amesema badala ya vijana kuangaika kutafuta viongozi kwenye simu ili kupata fursa za ajira au kazi zinanotolewa, wanatakiwa kuziomba fursa hizo kwa wingi ili wachaguliwe

Mhe Juliana Didas Masaburi Mbunge viti maalumu kupitia kundi la vijana

Aidha katika kuwasaidia vijana kuwa na miradi itakayowasaidia kuendesha jumuiya yoa Mhe Juliana amehaidi kuto mashine moja ya kufyatua tofari kwa vijana wa CCM wilaya ya Bunda.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavia Chacha Nyamigeko akiwa mgeni mualikwa katika baraza hilo amesema jumuiya ya umoja wa vijana ina changamoto ya ukosefu wa mradi wa kujiendesha ambpo amesema ili kuondokana na chanagamoto hiyo ameahidi pia kutoa mashine moja ya kufyatua tofari kwa jumuiya hiyo.

Diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavia Chacha Nyamigeko
Diwani wa kata ya Bunda stoo Mhe Flavia Chacha Nyamigeko

Awali akizungumza katika ufunguzi wa baraza hilo mwenyekiti wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Mohamed Msafiri amesema kulingana na ukosefu wa chanzo cha mapata katika jumuiya hiyo kinapelekea hata maudhurio katika mabaraza kuwa kidogo

Mwenyekiti UVCCM Bunda Mohamed Msafiri akijadiri jambo na Mhe Mbunge Juliana Masaburi, Picha na Adelinus Banenwa
Mwenyekiti wa umoja wa vijana chama cha mapinduzi wilaya ya Bunda Mohamed Msafiri

Friday, 14 July 2023

Nyatwali: miti yakatwa, Nyaraka za tathimini ya fidia kuchukuliwa mikopo kisa ugumu wa maisha

Baadhi ya miti iliyokatwa na wananchi wa Nyatwali kwa lengo la kuchoma mkaa ili wajikimu kimaisha, Picha na Edward Lucas

Zoezi la kuwaamisha wakazi wa kata ya nyatwali likiwa linaendelea katika hatua ya tathimini baadhi yao wanalia na hali ngumu ya maisha na njaa kutokana na kupigwa marufuku kufanya shughuri za uzalishaji na kulima mazao ya muda mrefu hali inayowapelekea kukata miti na kuingia kwenye mikopo umiza,

Na Edward Lucas

Ikiwa serikali bado inaendelea na mchakato wa kuwahamisha wakaazi wa  kata ya Nyatwali Halmashauri ya Mji wa Bunda, mapya yaibuka kwa wananchi kuanza kukata miti kwa ajili ya kuuza na kuchoma mkaa na kujitumbukiza kwenye mikopo kwa dhamana za nyaraka za fidia na tathimini ili kujikimu kimaisha.

Hayo yamebainika leo tarehe 13 July 2023 kupitia mahojiano ya Mazingira Fm na wananchi wa maeneo hayo mtaa wa Kariakoo wakati ilipowatembelea kwa lengo la kujua nini zaidi kinachoendelea katika zoezi la kuhamishwa.

Baadhi ya miti iliyokatwa na wananchi wa Nyatwali kwa lengo la kuchoma mkaa ili wajikimu kimaisha, Picha na Edward Lucas

Wamesema tangu ulipoanza mchakato wa kuhamishwa walielekezwa kutoendeleza makazi wala kutolima mazao ya muda mrefu jambo ambalo limepelekea baadhi kukosa uhakika wa chakula na makazi bora hivyo kujikuta wanaingia katika mikopo-umiza kwa kuweka dhamana nyaraka zao za fidia kwamba watarejesha baada ya kuwa wamelipwa fidia.

Hali hiyo imethibitishwa na Diwani wa Kata hiyo, Malongo Mashimo alipotafutwa na Mazingira Fm kwa njia ya simu na kusema kuwa kufuatia hali hiyo ameomba serikali iwasaidie wananchi kupata huduma ya mahindi ya bei nafuu na iharakishe mchakato kwani wameshindwa kujishughulisha na uzalishaji mali na shughuli zingine za maendeleo.

Malongo Mashimo Diwani wa Kata ya Nyatwali

Aidha katika hatua nyingine baadhi ya wananchi waliotathiminiwa maeneo yao yalioingia ndani ya maji maarufu kama ‘masanga’ wameishukuru serikali kwa kusikia kilio chao huku wale waliokosa nafasi hiyo kwa kigezo cha kukosa hati za maeneo yao wakiiomba serikali iangalie namna ya kuwasaidia kutokana na kuwepo kwa changamoto mbalimbali zilizokwamisha kupata hati hizo.

Mkazi wa kata ya Nyatwali

Thursday, 13 July 2023

Mwenge wa uhuru wateketeza zana haramu za uvuvi Bunda

zana haramu za uvuvi zilizoteketezwa na kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Ndgu Abdallah Shaibu Kaim eneo la Mwalo wa Kibra Bunda, Picha na Thomas Masalu

Mbio za mwenge kitaifa mwaka 2023 katika halmashauri ya wilaya Bnda imetembelewa miradi 7 ambapo miongoni mwa shughuli zilizofanyika ni uteketezaji wa zana haramu za uvuvi ikiwa ni jitihada za kulinda na kutunza mazingira.

Na Thomas Masalu

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 ameteketeza zana haramu za uvuvi zilizokamatwa hivi karibu na maafisa wa uvuvi wa Halmashauri hiyo katika mwalo wa Kibara Kata ya Kibara halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023 Ndgu Abdallah Shaibu Kaim, kulia na mkuu wa wilaya ya Bunda Mhe Dkt Vicent Anney Naano, katika moja ya mradi wa utunzaji wa mazingira uliozinduliwa na mwenge katika halimashauri ya wilaya ya Bunda, Picha na Thomas Masalu

Akiteketeza zana hizo, Abdalah Shaibu Kaim amesema serikali haiwezi kufumbia macho uvuvi haramu hivyo ni vyema wananchi wakaachana na shughuli ya uvuvi haramu maana hailipi.

Abdalah Shaibu Kaim Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2023

Aidha amewaomba wananchi kuendelea kuwa mabalozi wema katika utuzanji wa rasiliamali ili kizazi kijacho kifaidike na rasiliamali zilizopo.

Uteketezaji huo umefanyika leo katika eneo la mwalo wa Kibara ambapo pia choo cha matundu matano chenye lengo la uboreshaji wa mazingira kimezinduliwa.

Hiyo ikiwa ni miongoni mwa miradi kati ya miradi 7 iliyotembelewa na mwenge wa uhuru 2023 ndani ya halmashauri ya wilaya ya Bunda.

Tuesday, 11 July 2023

Mwl. James: waibueni watoto wenye mahitaji maalumu fulsa zipo

 

Mwl. James Masegwe mwalimu mkuu shule ya msingi Mazoezi katika eneo la mradi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalumu, Picha na Adelinus Banenwa

Wananchi watakiwa kutowaficha watoto wenye mahitaji maalumu kwa kuwa sasa serikali inatoa nafasi kubwa kwao katika sekta ya elimu

Na Adelinus Banenwa

Wito umetokewa kwa jamii wazazi na walezi mjini Bunda kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu Ili waweze kupata elimu itakayowasaidia katika kutimiza ndoto zao.

Hayo yamesemwa na James Masegwe Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Mazoezi wakati akizungumza na Mazingira Fm iliyofika shuleni hapo kuzungumza na Mwalimu huyo juu ya Changamoto zinazowakumba watoto wenye mahitaji maalumu.

Shule ya Mazoezi ni miongoni mwa shule za ziliyopo katika halmashauri ya mji wa Bunda inayowahudumia watoto wenye mahitaji maalumu.

Mwl. James Masegwe amesema hadi hivi sasa shuleni hiyo ina jumla ya watoto wenye mahitaji maalumu wapatao 86 ikiwa wavulana ni 54 na wasichana 32.

Aidha Mwl James amesema serikali imeleta mradi wa ujenzi wa Bweni kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu itakayochukua wanafunzi 80 litakaloghalimu shiling milioni 156  ambapokwa sasa bweni lipo katika hatua ya kuezeka.

Madarasa yatakayotumiwa na wanafunzi wenye mahitaji maalumu shule ya msingi Mazoezi, Picha na Adelinus Banenwa

Amesema changamoto kubwa kwa sasa ni mtazamo hasi kwa jamii kuweza kuwaibua watoto wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata haki yao ya kupata elimu.

Mwl. James Masegwe mwalimu mkuu shule ya msingi Mazoezi

Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyasura Magigi Kiboko amewataka wakazi wa kata hiyo kuipenda miradi inayoletwa kweny kata hiyo na kukubali kuchangia pale inapoitajika.

Magigi Mamwel Kiboko diwani kata ya Nyasura akikagua moja ya mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya unaotekelezwa kwenye kata yake, Picha na Adelinus Banenwa

Magigi Mamwel Kiboko diwani kata ya Nyasura

Monday, 10 July 2023

Matumaini bei ya pamba kupanda yazidi kufifia kwa wakulima mkoa wa Simiyu

 

Wakulima wa pamba kijiji cha Sapiwi mkoani Simiyu wakiwa katika kituo cha ununuzi wa pamba kwa ajili ya kuuza. Picha na Edward Lucas

Ikiwa ni takribani miezi miwili tangu kuzinduliwa msimu wa pamba 2023 hakuna hata senti moja iliyoongezeka kutoka katika bei elekezi iliyotangazwa na serikali ya shilingi 1,060 kwa kilo.

Wakizungumzia hali hiyo wakati wa mahojiano na Mazingira Fm iliyotembelea vituo hivyo hapo jana tarehe 9 July 2023 baadhi ya wakulima na viongozi wa vituo vya ununuzi wa pamba katika kijiji cha Lutubiga, Mkula na Sapiwi mkoani Simiyu wamesema hali hiyo imefanya baadhi ya wakulima wauze pamba yao kwa shingo upande baada ya kusubiri pasipo mafanikio wala dalili yoyote ya bei kuongezeka.

Elias Joseph ambaye ni Mwenyekiti wa AMCOS kijiji cha Sapiwi amesema  Mkoa wa Simiyu wanatumia mfumo wa makampuni na Vyama vya Ushirika AMCOS katika ununuzi wa pamba ujulikanao kama 'Simiyu Model' lakini tangu uanze msimu wa pamba hakuna dhana ya ushindani wa makampuni katika kuongeza bei isipokuwa ushindani umebaki ni kwa wakulima kuangalia ni kituo gani kina mzani wa kuaminika na iwapo kina fedha za kumlipa kwa wakati.

"Wakulima walianza kwa kusuasua wakiamini huenda bei inaweza kuongezeka kama ilivyokuwa mwaka jana ambapo wakulima walianza na bei ya shilingi 1,560 kwa kilo na baadaye ilipanda hadi kufikia 2,200 lakini kwa mwaka huu hadi sasa bei imebaki ile ile iliyotangazwa ya 1060 na wakulima wameona hakuna namna bora wauze ili waendelee na mambo mengine" alisema Mashaka Kwisotela ambaye ni Katibu wa AMCOS kijiji cha Mkula.

Mashaka Kwisotela, Katibu AMCOS ya Mkula akiwa kwenye kituo cha ununuzi wa Pamba akiendelea na zoezi


Wakulima kijiji cha Sapiwi wakiendelea na zoezi la uuzaji wa pamba. Picha na Edward Lucas


Saturday, 8 July 2023

Mazingira fm waipa tano TADIO kwa mafunzo

Muhariri wa Radiotadio Hilali Luhundwa akiwa anatoa mafunzo kwa wafanyakazi wa Radio Maingira Fm, Picha na Edward Lucas

Mtandao wa radio za kijamii Tanzania TADIO waendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka redio za kijamii namna ya kutumia mitandao ili iwe fulsa kwao,

Na Catherine Msafiri na Avelina Sulusi

Wito umetolewa kwa viongozi wa redio za kijamii kusimamia waandishi ili mafunzo ya matumizi ya redio mtandao  wanayoyapata yasaidie kuleta mabadiriko katika redio zao

Wito huo umetolewa Julay 7,2023 na Hilali Alexerder Luhundwa  ambaye ni muhariri wa Radiotadio iliyoko chini ya Mtandao wa radio za kijamii Tanzania TADIO  wakati akizungumza na Mazingira Fm alipofika kituoni hapo kwaajiri ya kutoa mafunzo ya namna ya kuchapisha habari katika mtandao.

lengo kuu likiwa ni kuziunganisha redio za kijamii zitumie jukwaa hilo kubadirishana habari.

Hilali  amebainisha kuwa kutokana na mafunzo wanayotoa wanatarajia kuona radio zinabadirika na kuwa kwenye mitandao ya kijamii lakini pia waandishi wanatumia mwanya huo kama fulsa kwao hasa ukizingati teknolojia inabadirika kila siku hivyo waandishi na redio zinalazimika kubadirika kulingana na teknolojia.

Mafunzo yakiendelea kwa waandishi wa Mazingira Fm
Hilali Alexerder Luhundwa  muhariri wa Radiotadio

Aidha amebainisha kuwa TADIO  kama Mtandao wa radio za kijamii Tanzania wamelazimika kuanzisha jukwaa la redio mtandao lengo kuu likiwa ni kuziunganisha redio za kijamii zitumie jukwaa hilo kubadirishana habari.

Hilali Alexerder Luhundwa  muhariri wa Radiotadio

Kwa upande wao waandishi wa habari wa kituo cha radio Mazingira Fm wameishukuru tadio kwa mafunzo waliyoyapata na  kutokana na mafunzo hayo wamejua namna ya kuchapisha habari kwenye mtandao pia kutumia mitandao ya kijamii kama fulsa  .

Aidha wameiomba  TADIO  kuendelea kutoa mafunzo haya ili yaendelee kuwajenga na kuendana na kasi ya mabadiriko ya technolojia duniani

Wandishi kutoka Mazingira Fm