Jeshi la
polisi wilaya ya Bunda Mkoani Mara linawashikilia Watu watatu kwa tuhuma za
mauwaji ya mwanamkea mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Bhoke mke wa matasu mwenye umri wa miaka 64
mkazi wa kijiji cha kyandege kata ya mgeta.
Tukio la kuuwawa
kwa mwanamke huyo limetokea alfajiri ya tarehe 16 mwezi huu wakati mwanamke
huyo akitoka chooni kujisaidia ndipo alipigwa na wauwaji hao na kitu chenye
ncha kali sehemu za mgongoni na shingoni.
Baada ya kutekeleza mauaji hayo watu hao hawakuchukuwa
kitu chochote kutoka kwa marehemu licha ya marehemu kuwa na fedha kiasi cha
shilingi laki moja ambapo imeelezwa kuwa chanzo cha mauji hayo ni imani za
kishirikina.
Hata hivyo Jeshi
la polisi wilaya ya bunda limetoa wito kwa wananchi kutoa taarifa mapema pindi
wanapoona hali kama hiyo ndani ya jamii.
No comments:
Post a Comment