Mkwasa aionya Simba - Mazingira FM

Mazingira Fm Live

Breaking News

Thursday 19 April 2018

Mkwasa aionya Simba


Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema wao hawana hofu hata kidogo na mechi dhidi ya watani wao Simba.

Simba itakutana na Yanga katika mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa Aprili 29 jijini Dar es Salaam.

Mkwasa amesema anaamini kama ni maneno, basi watani wao Simba wangekuwa na nafasi ya kuwa mabingwa kwa kuwa “wanachonga” sana.

“Suala la kutishia kutufunga ni hadithi tu, mpira hauko hivyo. Unajua wenzetu wanaongea sana, maana kama ingekuwa kuna kombe la kuzungumza, basi wao wangekuwa mabingwa.

“Tuna timu nzuri na tunaweza kupambana na kufanya vizuri, hakuna masuala ya kusema utafungwa na mwingine kujiamini kwa asilimia mia atashinda,” alisema.

Mashabiki wa Simba ndiyo walikuwa wanatamba kwa muda mrefu kutokana na kasi ya kikosi chao katika Ligi Kuu Bara, lakini Yanga wamepata morali baada ya kikosi chao kuingia katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa kuing’oa Wolayta Dicha ya Ethiopia.

No comments:

Post a Comment