Saturday, 21 October 2017

Bodi ya filamu tanzania yatuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha muigizaji nguli wa filamu shamila mfikirwa.

Bodi ya Filamu Tanzania imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Muigizaji nguli Shamila Mfikirwa.
Katika Salamu zake kwa Rais ya Shirikisho la Filamu Tanzania Bw. Simon Mwakifamba, Mwenyekiti wa chama cha Waigizaji Ndugu Elia Mjata na wanafamilia wa filamu na uigizaji kwa ujumla Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Bi.Joyce Fissoo amesema amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za msiba huo.
“Kwa niaba ya Bodi nachukua fursa hii kutoa pole nyingi sana kwa familia ya marehemu kutokana na kuondokewa na mpendwa wao, pia Bodi imeguswa na msiba huo na inawaombea wanafamilia kwa Mungu kuwa na moyo wa subra katika kipindi hiki kigumu” alisema Bi.Fissoo.
Mwigizaji Shamila Mfikirwa maarufu kama ‘Shamila’ amefariki dunia katika Hospitali ya Occean Road Jijini Dar es Salaam tarehe 20 Oktoba, 2017 alipokuwa akipatiwa matibabu.
Innalilah Wainna Ilayhi Rajiun.
Imetolewa na

Bodi ya Filamu Tanzania.

Wazazi watakiwa kuacha kutuma watoto wao usiku dukani

Zikiwa zimesalia wiki moja wanafunzi wa kidato cha nne nchini kote kuanza mtihani wao wa taifa wazazi na walezi wametakiwa kuwa na desturi ya kuwalea watoto wao katika maadili mema na kuacha kuwatuma kwenda kununua mahitaji mbalimbali dukani nyakati za usiku kwani kufanya hivyo ni kutoa mwanya kwa watoto hao kukutana na watu wanaoweza kukatisha ndoto zao kwa kuwapatia mimba.
Hayo yamesemwa jana na mgeni rasmi katika mahafari ya 24 katika shule ya sekondari bunda mheshimiwa diwani wa kata ya kabarimu Pastory Ncheye.
Amesema suala la mimba linatokana na wazazi kutowajengea malezi mazuri watoto wao, na kutolea mfano kuwa mzazi anapomtuma mtoto kwenda kufanya biashara usiku au kununua bidhaa usiku dukani inapelekea watoto hao kukutana na watu wanaowashawisha kushiriki nao kufanya ngono hatimae kupata mimba.
Aidha amewatahadharisha wanafunzi kuacha kujihusisha na vitendo vya ngono kwani kupata mimba ni majaliwa lakini watambue kwamba kuna gonjwa hatari la ukimwi.
Mheshimiwa ncheye katika mahafari hayo ameaidi kushirikiana na shule hiyo kurekebisha gari la shule lililoaribika kwa  muda mrefu hivyo kuitaji fedha zaidi ya shilingi milioni moja kukamilika.
Pamoja na hayo pia ncheye ameaidi kuwapelekea miche ya miti ili kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanaendelea kuwa mazuri na ya kupendeza, na kuwasifu kwa jitihada walizozifanya za usafi wa mazingira.
Kwa upande wake mwalim mkuu wa shule hiyo Machota Kora katika risala yake amesema kuwa wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya upungufu wa matundu ya vyoo, vyumba vya madarasa, pamoja na uzio katika mabweni ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita.
Hata hivyo amewaomba wazazi na walezi kushirikiana na walimu katika kuwalea watoto kwakuwa wao wenyewe hawawezi na ndiyo maana katika shule hiyo jumla ya wanafunzi watatu waliotakiwa kuhitimu na wanzao walikatisha masomo yao kwa kupata mimba.



Afisa mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick steven Kaduri apinga takwimu ya mifugo 770 kufa.

Siku chache baada ya kituo hiki  kuripoti habari kuhusu mifugo zaidi ya 700 kufa kwa tatizo la kukosa maji na majani kwa muda mrefu, hatimae leo mkuu wa idara ya mifugo na uvuvi wa halmashauri ya mji wa bunda Mkoani Mara bwana Rick steven Kaduri amejitokeza na kupinga ukweli wa taarifa hiyo licha ya kukiri kuwa mifugo imekufa.

Amesema kuwa ni kweli mifugo imekufa katika halmashauri ya mji wa bunda, lakini ameshangazwa na idadi iliyotajwa ya mifugo zaidi ya  700 kufa huku akisema kuwa kwa taarifa walizonazo kama halmashauri nzima ni zaidi ya mifugo 1000 imekufa kwa kukoswa maji na majani kwa muda mrefu.
Amesema taarifa kama hizo zilisikika tena guta kuwa zaidi ya ng’ombe 3000 wamekufa lakini bado wanazidi kuzifanyia uchunguzi kubaini ukweli wake.
Amesema tatizo la mifugo kufa imetokana na ukame wa muda mrefu huku akitaja kuwa wafugaji waliokuwa na ng’ombe wenge ndio waathirika wakubwa hivyo amewakumbusha wafugaji kufuga kisasa ili waweza kumudu hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi.
Hivi karibuni mtandao huu umewatembelea wafugaji wa kijiji na kata ya rwabu kutaka kujua hali ya mifugo ambapo mwenyekiti wa kijiji hicho bwana Gelad Kuzenza,  alisema kuwa kwa makisio ya chini walikuwa na ng’ombe 1500 na lakini  kwa sasa wamebaki 700 huku akieleza kuwa  bei ya ng’ombe imeshuka hadi shilingi 15,000 huku wanunuzi wakisusia kununua mifugo hiyo wakati mwingine kutokana na hali ya ya kudhoofika zaidi.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha wafugaji kanda ya ziwa kwa maana ya mikoa ya  Mara, simiyu shinyanga, mwanza geita na Kagera bwana Mrida mshota amekiri kuwepo kwa tatizo la mifugo mingi kufa kwa ukame na hasa ng’ombe ambapo amesema kuwa wameshaanza mikakati ya kukabiliana na tatizo hilo kwa kuanzisha mashamba ya majani kwa ajili ya mifugo yao.
Amesema zoezi hilo sio la muda mfupi kwa kuwa watanzania wengi na hasa mikoa ya kanda ya ziwa bado wanafuga ng’ombe wa kienyeji na wana mifugo mingi.
Amewataka wafugaji kuanza kubadilika kwa kufuga kisasa ili waweze kuendana na mabadiliko ya tabia ya nchi.



Jumla ya wazee 235 katika kata ya neruma wilayani Bunda Mkoani Mara wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu

Jumla ya wazee 235 katika kata ya neruma wilayani Bunda Mkoani Mara  wamepatiwa vitambulisho vya msamaha wa matibabu lengo ikiwa ni kuhakikisha wazee wanatambuliwa na kupewa fursa ya kushiriki katika mambo yanayohusu maisha yao ya kila siku.

Akisoma taarifa ya utoaji wa huduma za afya na stawi wa jamii Kwa mgeni Rasmi Kaimu Afisa Ustawi wa Jamii wilaya ya bunda Liberatus Kazana katika maadhimisho ya siku ya wazee Duniani yaliyofanyika Katika kijiji cha Neruma kata ya neruma Oktoba 20 amesema Halmashauri ya wilaya ya Bunda inajumla ya wazee 9,994 waliona miaka 60 na kuendelea.

Kazana Amesema kunachangamoto mbalimbali katika uendeshaji wa huduma za afya na hasa katika kuwahudumia wazee huku gharama za uendeshaji wa huduma za msamaha zimekuwa kubwa katika vituo vya kutolea huduma za afya hiyo ikitokana na idadi kubwa ya wagonjwa wanaohitaji msamaha kama vile akina mama wajawazito,watoto chini ya miaka mitano,walemavu na wazee.


Kwa upande mgeni rasmi katika maadhimisho hayo ambaye ni Katibu Tawala wa wilaya ya Bunda Masalu Kisasira amesema wao kama serikali wanatambua changamoto hizo hivyo ameahidi kuzifanyia kazi huku akiwasihi wazee kuwa kioo kizuri kwa watoto wao kwa kuwaonya na kuwashauri ili kuwawezesha watoto wao kuwa na misingi bora ya maisha.