Mazingira Fm Nikituo Cha Radio Kiliopo Wilayani Bunda Mkuoni Mara,
Monday, 10 February 2025
Bunda: Mwili wa mvuvi aliyezama ziwa Victoria wapatikana
11 February 2025,
Baadhi ya wananchi na wanafamilia wakiwa kando ya ziwa Victoria wakishuhudia zoezi la utafutaji wa aliyezama maji (picha na Yohana)
Aliyepotelea ziwani akiwa kwenye shughuli ya uvuvi, mwili wake umepatikana ikiwa ni siku ya tano tangu alipotoweka.
Na Edward Lucas
Kusekwa Fanuel Rufundya (31) mkazi wa kata ya Guta halmashauri ya mji wa Bunda aliyepotelea ziwani akiwa kwenye shughuli ya uvuvi, mwili wake umepatikana ikiwa ni siku ya tano tangu alipotoweka
Mwili huo umepatikana majira ya alasiri baada ya jitihada za wavuvi na wananchi katika zoezi la utafutaji tangu tarehe 7 Feb 2025 majira ya saa 2:00 asubuhi lilipotokea tukio hilo wakati marehemu na wenzake wawili wakiwa kwenye mtumbwi kwa uvu
Makongo Moni ni mmoja wa wavuvi waliokuwa na marehemu wakati wa tukio, ameiambia redio Mazingira Fm kuwa wakati wakiwa kwenye ‘mashua’ wanaelekea zilipo ndoano zao ndipo upepo ulizidi na mawimbi makali vilitokea jambo lililosababisha chombo chao kujaa maji na kuanza kuzama na katika jitihada za kujiokoa marehemu alishindwa kutokana na kukosa uzoefu wa kuogelea
Makongo Moni ni mmoja wa wavuvi waliokuwa na marehemu
Sunday, 9 February 2025
Bunda: Mvuvi atumbukia ziwa Victoria, siku ya tatu hajapatikana
9 February 2025,
Baadhi ya wananchi na wanafamilia wakiwa kando ya ziwa Victoria wakishuhudia zoezi la utafutaji wa aliyezama maji (Picha na Yohana)
By Edward Lucas
Mtu mmoja Aliyefahamika kwa jina la Kusekwa Fanuel Rufundya (31) mkazi wa mtaa wa Ihale kata ya Guta anahofiwa kufariki dunia kwa kuzama ndani ya maji wakati akiwa katika shughuli za uvuvi ziwa victoria kata ya Guta halmashauri ya mji wa Bunda mkoani Mara.
Mwenyekiti wa mtaa wa Guta Mjini, Steven Malweta Mabusi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo Ijumaa tarehe 7 Feb 2025 majira ya saa 02:00 asubuhi wakati mtu huyo akiwa kwenye mashua (mtumbwi) na wenzake wawili wakiendelea na shughuli za uvuvi ndipo ghafla alitoweka na juhudi za wenzake kuanza kumtafuta zilizanza kwa haraka bila ya mafanikio yoyote
Steven Malweta Mabusi, mwenyekiti wa mtaa
Misoji Rufundya ni Mama mkubwa wa Kusekwa Rufundya ambaye yuko katika eneo la tukio ameeleza kwa namna alivyopokea taarifa ya kijana wao kuzama majiniI
Misoji Rufundya
Saturday, 8 February 2025
Mikoa, halmashauri zapewa maelekezo vita dhidi ya ukeketaji
8 February 2025, 10:18 pm
Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dr. Doroth Gwajima
Waziri Gwajima ameiagiza mikoa yote inayoongoza kwa ukeketaji nchini kutenga bajeti za kutekeleza afua za kupinga ukeketaji ikiwa ni pamoja na kuwahudumia manusura wa ukatili wa ukeketaji na ukatili mwingine.
Na Adelinus Banenwa
Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dr. Doroth Gwajima ameiagiza mikoa yote inayoongoza kwa ukeketaji nchini kutenga bajeti za kutekeleza afua za kupinga ukeketaji ikiwa ni pamoja na kuwahudumia manusura wa ukatili wa ukeketaji na ukatili mwingine ikiwemo kuwawezesha watoa huduma kuwafikia wahanga kwa urahisi.
Dr Gwajima ameyasema hayo leo Feb 8, 2025 wilayani tarime kwenye maadhimisho ya siku ya kupinga ukeketaji Duniani
Waziri Dr Doroth Gwajima na viongozi wengine wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa kituo jumuishi cha huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili Wa kijinsia Nyamwaga Tarime
Maadhimisho hayo ameambatana na uzinduzi wa kituo jumuishi cha huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili eneo la Nyamwaga Tarime kilichogharimu shilingi milioni 186 kwa ufadhili wa shirika la umoja wa mataifa linalojihusisha na idadi ya watu duniani UNFPA ambapo lengo kuu la kituo hicho ni kutoa huduma za pamoja kwa wahanga na manusura wa ukatili ndani ya jengo moja.
Kutuo hicho tangu kilipoanza kufanya kazi mwezi July 2024 hadi sasa manusura wapatao 325 wakiwemo watoto 204 wamehudumiwa ambapo kwa mujibu wa takwimu hizo watoto ndiyo wanaofika kituoni hapo kwa wingi kupata huduma.
Waziri Dr Doroth Gwajima akifungua kibao kuashiria ufunguzi wa kituo jumuishi cha huduma kwa wahanga wa matukio ya ukatili Wa kijinsia Nyamwaga Tarime
Kituo hicho kinatoa huduma za afya, msaada wa kisheria pamoja na ustawi wa jamii lengo likiwa ni kutoa huduma za pamoja kwa manusura wa ukatili ambapo UNFPA kadhalika wamejenga jengo kama hilo katika mkoa wa Shinyanga.
Pia Mhe Gwajima amesema mbinu mpya ya Ukeketaji imeibuka hasa maeneo ya mipakani ambapo makundi ya vijana wa kike huvushwa mipakani na kupelekwa nchi jirani kwa ajiri ya kufanyiwa ukeketaji na kisha kurudishwa nchini bila kubainika pia mangariba vivyo hivyo.
Katika kukabiliana na mbinu hizo mhe Waziri Gwajima ameelekeza vituo vyote jumuishi vikae na kuandaa taarifa yao ya pamoja itayohusisha wataalamu wa afya. Jeshi la polisi na ustawi wa jamii ili muhutasari wao uambatanishwe na MTAKUWA kisha upelekwe ofisi za wilaya kisha mkoani kisha upande kwenda wizarani na wizara zitakaa na kushauri wanasheria kufanya marekebisho ya sheria ya ukeketaji na masuala mengine kama yatakavyokuwa yamependekezwa kutoka kwenye vituo hivyo.
Sauti Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi maalumu Dr. Doroth Gwajima
Awali akizungumza katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara Kanal Evance Mtambi ameiagiza halmashauri ya wilaya ya Tarime kupitia mapato ya ndani kujenga nyumba salama kwa ajili ya watoto wanaofanyiwa ukatili.
Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara
Pia Dr Naano kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mara ameagiza kutolewa kwa elimu Maafisa wa jeshi la polisi wanaohusika na kuhudumia wahanga wa ukatili ili wawe na mtazamo mmoja katika kushughulikia kesi hizo za ukatili.
Sauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano
Mark Bryan Schreiner mwakilishi mkazi wa UNFPA nchini Tanzanian amesema tatika kupambana na ukatili wa kijinsia ikiwemo ukeketaji na ndoa za utotoni kunahitajika juhudi za pamoja kati ya wanawake wanaume watoto vijana pamoja na serikali
Mark amesema kupitia program ya chaguo langu haki yangu imeonesha mshikamano na utayari wa serikali katika kutokomeza ukatili huo kwenye jamii.
Michael Marwa kutoka C-SEMA na Valerian Mgani kutoka ATFGM MASANGA taasisi ambazo zimejikita katika kutoa elimu ya ukatili wa kijinsia kwa akinamama na watoto hasa wenye ulemavu GBV wamesema hotuba ya Mhe Waziri wameipokea kwa mikono miwili kutokana kwa kuwa inaonesha namna serikali kwa kushirikiana na wadau wameweza kupunguza kiwango cha ukeketaji nchini na mipango itakayowezesha kuendelea kusaidia kushusha kiwango cha ukeketaji na hata kubaki asilimia 0
Sauti za Michael Marwa kutoka C-SEMA na Valerian Mgani kutoka ATFGM MASANGA
Thursday, 6 February 2025
Kamati ya fedha Bunda TC yakagua miradi, yaipa tano Bunda Mjini Sec
6 February 2025,
Nyumba ya walimu Bunda mjini Sekondari ambayo itagharimu milion 100 hadi kukamilika kwake
Wananchi watakiwa kulinda miradi ili iweze kudumu na kuhudumia kizazi cha sasa na hata kile kijacho
Na Adelinus Banenwa
Kiasi cha shilingi milioni 88 kimeshatumika kati ya shilingi milioni 100 kwenye ujenzi wa Nyumba ya walimu shule ya sekondari Bunda mjini mkoani Mara
Mkuu wa shule ya sekondari ya Bunda mjini amesema nyumba hiyo imejengwa katika mfumo wa Nyumba mbili ndani ya moja ambayo familia mbili za walimu wataishi pindi itakapokamilika.
Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka, Akisaini kitabu cha wageni baada ya ukaguzi
Ufafanuzi huu umetolewa kwa kamati ya fedha ya halmashauri ya mji wa Bunda iliyofika shuleni hapo kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo wa nyumba ya mwalimu.
Katika ujumbe wake mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka mbali na kupongeza mkuu wa shule kwa usimamizi mzuri wa mradi amemtaka kukamilisha ujenzi huo kwa wakati ili nyumba hiyo iweze kutumika.
Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Bunda na diwani wa kata ya Sazira Mhe Michael Kweka
Kwa upande wake mkurugenzi wa mji wa Bunda Juma Haji ametoa wito kwa wananchi kuhakikisha wailinda miundombinu inayoletwa na serikali katika maeneo yao ili iendelee kuhudumia kizazi cha sasa na hata kijacho.
Sauti ya mkurugenzi wa mji wa Bunda Juma Haji
Monday, 3 February 2025
Zaidi ya watu 2700 wafikiwa wiki ya sheria Bunda
3 February 2025,
Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda, katika kilele wiki ya sheria
Wananchi zaidi ya 2700 wamefikiwa wiki ya sheria wilayani Bunda baada ya kufika katika vituo vilivyokuwa vimeainishwa na wadau wa mahakama.
Na Adelinus Banenwa
Wananchi zaidi ya 2700 wamefikiwa wiki ya sheria wilayani Bunda baada ya kufika katika vituo vilivyokuwa vimeainishwa na wadau wa mahakama.
Hayo yamesemwa na Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Bunda katika kilele cha maadhimisho wiki ya sheria ambapo kwa wilaya ya Bunda maadhimisho hayo yakifanyika leo Feb 3, 2025 kwenye viwanja vya mahakama ya wilaya ya Bunda.
Sauti ya Mulokozi Kamuntu hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya BundaMkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano katika kilele wiki ya sheria
Katika maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano akiwa mgeni wa heshima ameipongeza mahakama wilayani Bunda kwa kufuata sheria katika kutekeleza majikumu yake hali ambayo amedai inapunguza tabia ya mahakama kulalamikiwa katika utendaji wa haki.
Baadhi aya watumishi wa mahakama wilayani Bunda katika kilele wiki ya sheria
Pia amewashukuru wadau wote wa sheria ikiwemo ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, ofisi ya mawakili chini ya TLS huku akiwanyooshea vidole baadhi ya mawakili wasiyokuwa waaminifu katika utendaji wao wa kazi .
Sauti Mkuu wa wilaya ya Bunda Dkt Vicent Naano
Friday, 31 January 2025
Mkurugenzi TECTO community aelezea fursa za ajira kupitia utalii kanda ya ziwa
31 January 2025,
Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias
“Kanda ya ziwa inavivutio vingi vya utalii mbavyo ni fursa Katika kutatua tatizo la ukosefu wa ajira nchini”
Na Catherine Msafiri,
Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias ameeleza kuwa Kanda ya ziwa Kuna fursa nyingi zinazowezakupunguza tatizo la ukosefu wa ajira kutokana na uwepo wa vivutio vingi vya utalii ikiwemo pori la akiba kijereshi ,Hifadhi ya Taifa Serengeti na makumbusho ya baba wa Taifa mwitongo Butiama.
Ameeleza hayo alipofanya mahojiano kwenye kipindi Cha uhifadhi na utalii kinacholushwa kupitia radio Mazingira fm ambapo madam iliangazia juu ya kuvifahamu vivutio vya utalii vinavyopatikana akanda ya ziwa.
Mkurugenzi wa TECTO community company Bw.Juma Elias Elias akiwa ofisin kwake
Bw. Juma amesema kuwa kama watu wakijikita kuwekeza katika sekta ya utalii itasaidia kupunguza ukosefu wa ajira kwakua kuna fursa za biashara za kitalii kama uuzaji wa vinyago ,matunda , utengenezaji wa matenti ya kitalii,vilimo vya utalii na utalii wa kiutamaduni
Sauti ya Juma Elias Mkurugenzi wa TECTO community Company akielezea fursa za kitalii
Aidha ameshauri kuwa watu wanapaswa kujitoa kusoma masuala ya utalii na wale waliosomea wajikite katika vivutio vya Kanda ya ziwa kutasaidia kufungua shughuli za Utalii Kwa ukubwa Kanda ya ziwa
Sauti ya Juma Elias Mkurugenzi wa TECTO community Company akitoa ushauri
Ni katika Mahafali ya Kidato cha 4 shule ya Sekondari Kabasa, Kambarage Wasira akiwa mgeni rasmi atoa milioni 1 (1,000,000/=Tsh) kukabili sehemu ya changamoto katika shule hiyo.
Wahitimu wa kidato cha 4 Sekondari Kabasa wakifanya yao mbele ya wageni waalikwa.Shangwe kama lote kwa walimu na wanafunzi Kabasa SekondariMiongoni mwa wageni waalikwa ilikuwa ni pamoja na walimu kutoka shule mbalimbali wilaya ya BundaKambarage Wasira akizungumza katika mahafali ya 17 shule ya Sekondari Kabasa. Picha na Edward Lucas
Na Edward Lucas
Ikiwa ni wiki moja imepita tangu Kambarage ashiriki mahafali ya darasa la saba shule ya msingi Kunzugu na kutoa ahadi ya ‘Printa’ yenye thamani ya milioni 1 na laki 2 (1,200,000/=) hii leo ilikuwa ni zama ya Sekondari Kabasa akiwa mgeni rasmi tena.
Katika mahafali hayo, Kambarage Wasira ametoa shilingi milioni 1 ili kusaidia sehemu ya changamoto zinazoikabiri shule hiyo.
Sauti ya Kambarage WasiraGodfrey Maige Maduhu, Mkuu wa shule ya Sekondari Kabasa. Picha na Edward Lucas
Awali akisoma taarifa ya shule, Mkuu wa shule hiyo, Godfrey Maige Maduhu amebainisha changamoto mbalimbali zinazoikabiri shule hiyo kuwa ni pamoja na ukosefu wa bwalo, maktaba, upungufu wa walimu na upungufu wa matundu ya choo 24 huku akiipongeza serikali ya awamu ya sita kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwani shule hiyo ina madarasa ya ziada 6
Sauti ya Godfrey Maige MaduhuGrace Raymond akisoma risala ya wahitimu kidato cha 4 Sekondari Kabasa ikibainisha baadhi ya changamoto walizokumbana nazoSauti ya Grace Raymond
Baadhi ya viongozi wa NMB na serikali wakipeana mikono baada ya kukabidhi Madawati, Picha na Adelinus Banenwa
Katika kuadhimisha wiki ya wateja banke ya NMB tawi la bunda wametoa msaada wa madawati 100 kwa sule ya msingi ya nyasura iliyopo kata ya nyasura halamshauri ya mji wa bunda mkoani mara.
Na Adelinus Banenwa
Katika kuadhimisha wiki ya wateja banke ya NMB tawi la bunda wametoa msaada wa madawati 100 kwa sule ya msingi ya nyasura iliyopo kata ya nyasura halamshauri ya mji wa bunda mkoani mara.
Akizungumza katika hafla ya kukabidhi madawati hayo mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho amesema banki hiyo imekuwa ikishiriki katika shughuli mbalimbali za kijamii kama vile sekta ya elimu, afya na uelimishaji wa mambo mbalimbali.
Amesema katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa mteja wamewiwa kutoa msaada huo kwa shule ya Nyasura kutokana na mahitaji yake ambapo dawati 100 zilizotolewa zimegharimu shilingi 12 milioni.
Mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho, Picha na Adelinus BanenwaSauti ya mkuu wa taasisi za serikali na taasisi binafsi banki ya NMB William Makoresho
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano ameishukuru bank ya NMB kwa kutoa msaada huo huku akibainisha kwa wilaya ya Bunda inaupungufu wa madawati elfu 16 huku halmashauri ya mji wa Bunda ikiwa na upungufu wa madawati elfu 6 .
Mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano, Picha na Adelinus BanenwaSauti ya mkuu wa wilaya ya Bunda Dr Vicent Anney Naano,
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyasura mwalimu Benard Ngero Paul amesema ujio wa madawati hayo kama msaada kutoka NMB utapunguza changamoto ya uhaba wa madawati japo bado yanaitajika madawati mengi kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi walioko shuleni hapo.
Mwalimu Benard amesema shule ya nyasura ina wanafunzi wapatao 1775 ambapo wasichana ni 985 na wavilana ni 790 ambao wanaitaji madawati 591 huku yaliyopo ni 197 huku upungufu ukitajwa ni madawati 394.
Aidha amebainisha changamoto nyingine ni matundu ya vyoo ambapo kwa mahitaji ni matundu 60 ya vyoo ila yaliyopo ni 12 tu.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Nyasura mwalimu Benard Ngero Paul